Home LOCAL MAAFISA LISHE WAHIMIZWA KUWA WABUNIFU KATIKA KUFANYA TAFITI MAENEO YA TIBA LISHE...

MAAFISA LISHE WAHIMIZWA KUWA WABUNIFU KATIKA KUFANYA TAFITI MAENEO YA TIBA LISHE NA AFYA YA JAMII,

Na: WAF – Dar es Salaam

Maofisa Lishe nchini wametakiwa kuwa wabunifu katika kufanya tafiti kwenye maeneo ya tiba lishe na afya ya jamii kwa ujumla ili kuleta manufaa nchini

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mafunzo na Elimu ya Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe nchini Dkt. Esther Nkuba wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa  chama cha Wanataaluma wa Lishe Tanzania  uliofanyika jijini Dar es Salaam

Dkt. Nkuba amesema ni lazima wawe wabunifu ili chama chao kionekane bora kwa kuibua mambo ya msingi ambayo yatakayo leta tija katika Taifa.

“Inabidi tujisimamie, ni lazima tuwe wabunifu ili chama chetu kionekane kwa kuibua mambo ya msingi ambayo yataleta tija katika taifa letu”amesema Dkt. Nkuba

Aidha,  Dkt. Nkuba amewaasa Maafisa lishe kuhakikisha huduma za lishe zinazotelewa nchini ziwe na ubora wa  na kuzingatia maadili ili kuleta tija kwa wagonjwa

“Hakikisheni huduma za lishe zinatolewa kwa ubora wa hali ya juu na kwa kuzingatia maadili ya taaluma zenu “amesema Dkt. Nkuba

Hata hivyo Dkt. Nkuba amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mbele katika kujitoa kupambana na utapiamlo nchini na kuhakikisha lishe inaenda vizuri katika nchi yetu,

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za lishe kutoka Wizara ya Afya Bi. Grace Moshi amewataka maafisa hao kufanya kazi kwa kujitoa na yenye ubora wa hali ya juu kama anavyo himiza Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu,

“Naomba tujisimamie, tuhakikishe  tunatoa huduma bora za tibalishe na afya ya jamii kwa ujumla katika vituo vyetu ili kuhakikisha vina simama sawasawa  “amesema Grace Moshi

Previous articleRAIS SAMIA ASISITIZA USHIRIKIANO NA VYAMA VYOTE VYA SIASA
Next articleWIZARA YA AFYA YAPOKEA VIFAA VYA TEHAMA VYENYE THAMANI YA MILIONI 200
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here