Home Uncategorized KMC YAIFUATA KAGERA SUGAR NA GEITA GOLD FC IKIWA NA NYOTA WAKE...

KMC YAIFUATA KAGERA SUGAR NA GEITA GOLD FC IKIWA NA NYOTA WAKE 24

 

Na; Stella Kessy, DAR

KIKOSI cha wachezaji 24, Benchi la ufundi pamoja na viongozi wa KMC FC  wanaondoka Jijini Dar es Salaam leo April 13 kuelekea mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara dhidi ya Kagera Suger utakaopigwa Jumapili ya Aprili 17 katika uwanja wa Kaitaba mkoani humo.

Akizungumzia na blog hii Afisa Habari na Mawasiliano wa KMC FC ,Christina Mwagala amesema kuwa kikosi chao kitashuka tena dimbani   dhidi ya Geita Gold  FC Aprili 23 katika mchezo wake utakaopigwa katika Dimba la  uwanja wa Nyankumbu.

Ameongexa kuwa kikosi chao kina maandalizi     vizuri chini ya kocha Mkuu Thierry Hitimana ya kuzisaka alama sita muhimu katika Timu hizo zilizopo kanda ya Ziwa.

Kikosi hicho kitakuwa na michezo mwingine dhidi ya Kagera Sugar pia kikosi cha KMC kinaendelea kujiimarisha ikiwa ni mara baada ya kutoka sare ya bila kufungana kwenye mchezo uliopita dhidi ya Namungo ambao ulichezwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam Aprili tatu mwaka huu.

Ameongoza kuwa yimu timu imejipanga kwenda kufanya vizuri kwenye michezo hiyo kwa  kanda ya Ziwa licha ya kwamba Kagera na Geita ni Timu nzuri na kwamba zimekuwa zikifanya vizuri kwenye michezo yake.

“KMC tunakwenda Kanda ya ziwa kesho, kutafuta alama sita kutoka kwenye Timu ya Kagera Sugar pamoja na Geita, tunafahamu kuwa Timu hizo ni nzuri na zimekuwa na matokeo mazuri kwenye michezo yao, lakini hiyo haituzuii Manispaa ya Kinondoni tukashindwa kupata alama zote kwasababu zipo ndani ya uwezo wetu.

“Tunawachezaji bora na wenye uwezo wakuipa Timu matokeo kwenye mazingira yoyote yale, sikuzote Timu yetu ni imara haijalishi hatujapata matokeo mazuri hivi karibu kwenye michezo mitatu iliyopita, hivyo tunahitaji ushindi kwenye michezo yetu, tunakwenda kwa tahadhari kubwa huku tukimtanguliza mwenyezi Mungu.

Kwaupande wa afya za wachezaji wote ziko vizuri , wanahari na morali , licha ya kuwa tutakuwa ugenini, lakini tunakwenda kuipambania Timu yetu, tunahitaji  kuwapa furaha mashabiki zetu, Manispaa yetu ya Kinondoni, na Watanzania wote ambao wanatusapoti, na kikubwa zaidi hatufikirii michezo ambayo ilishapita badala yake tunafokasi kwenye michezo iliyopo mbele yetu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here