Home Uncategorized KMC :TUPO GADO KUIKABILI NAMUNGO KESHO

KMC :TUPO GADO KUIKABILI NAMUNGO KESHO

Na: mwandishi wetu.

KIKOSI cha KMC FC leo kimefanya maandalizi yake ya mwisho kuelekea katika mchezo wake wa Ligi kuu ya NBC Soka Tanzania Bara dhidi ya Namungo utakaopigwa kesho katika Uwanja wa Uhuru  jijini Dar es Salaam saa 10:00 jioni.

Akizungumza na Green waves media afisa habari na Mahusiano wa KMC FC Christina Mwagala amesema kuwa Kikosi chao ambacho kipo  chini  ya Kocha Mkuu Thierry Hitimana hadi sasa imejiandaa vema kweye mchezo huo licha ya kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kwamba timu ya Namungo imekuwa ikifanya vizuri katika michezo yake lakini ubora wa wachezaji pamoja na Benchi zima la ufundi litahakikisha kuwa alama tatu muhimu zinapatikana.

“Tumetoka kupoteza michezo miwili mfululizo, na tunakwenda kwenye mchezo mwingine tukiwa nyumbani, hii ninafasi kwetu ya kusahihisha makosa ya awali na kwamba Kocha Mkuu Hitimana katika kipindi hiki ambacho Timu zilikuwa kwenye mapumziko kupisha kalenda ya FIFA amefanya maboresho kwenye maeneo ambayo aliona yanachangamoto ambazo zilikosesha Timu kupata matokeo mazuri, hivyo mashabiki zetu watarajie kupata burudani.

Hata hivyo kwa kipindi kirefu hatujatumia uwanja wetu halisi wa nyumbani, na sasa tunarejea kwenye mchezo  dhidi ya Namungo, hivyo Tunaipongeza TPLB kwa ushirikiano mkubwa waliotuonesha kwa kipindi chote hicho na sasa tunakwenda kesho tukifahamu kabisa mchezo utakuwa mgumu lakini KMC FC tumejipanga kuondoka na alama tatu muhimu.

Aidha Klabu ya KMC FC inawasihi mashabiki kujitokeza kwa wingi siku ya kesho kwenye mchezo huo muhimu ambao wachezaji wamejiandaa vizuri kuhakikisha kwamba wanatoa burudani iliyoambatana na ushindi, ukizingatia kuwa itakuwa siku ya wekeand.
Previous articleMAHIMBILI ASEMA SERIKALI INAENDELEA KUSAMBAZA GESI ASILIA MAJUKUMU
Next articleSTAMICO YAZIDI KUTANGAZA BIDHAA MPYA YA MKAA MBADALA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here