Home LOCAL KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AIPONGEZA RUWASA LUTEKELEZA MRADI WA MAJI NANGOMBA...

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AIPONGEZA RUWASA LUTEKELEZA MRADI WA MAJI NANGOMBA KWA WELEDI

Sehemu ya mradi wa maji wa Kangomba wilayani Nanyumbu mkoa wa Mtwara ambao umeanza kutoa huduma kwa wakazi zaidi ya 5,151 wa vijiji viwili vya Kangomba na Mjimwema uliotekelezwa na Wakala wa usambazaji maji safi na usafi wa mazingira(Ruwasa)kwa gharama ya Sh.196,430,118.06



Meneja wa Ruwasa wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara Mhandisi Simon Mchucha akitoa taarifa ya utekelezaji na usimamizi wa mradi wa maji Nangomba wilayani humo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 Sahil Geraruma(hayupo pichani)wakati Mwenge wa Uhuru ulipofika katika mradi huo.


Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 Sahil Geraruma katikati,akikagua sehemu ya ujenzi wa mradi wa maji wa Kangomba wilayani Nanyumbu,kushoto Meneja wa Ruwasa wilayani humo Mhandisi Simon Mchucha na kulia Mkuu wa wilaya Mariam Chaurembo.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 Sahil Geraruma kushoto, akimsikiliza Meneja wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)wilaya ya Nanyumbo Simon Mchucha katikati kuhusiana na mradi wa maji safi na salama wa Nangomba unaohudumia vijiji viwili vya Nangomba na Mjimwema,kulia Mkuu wa wilaya hiyo Mariam Chaurembo.


Kaimu Meneja wawakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)mkoa wa Mtwara Mhandisi Cosmas Komba katikati aliyevaa shati jeusi,Meneja wa Ruwasa wilaya ya Nanyumbu Simon Mchucha wa pili kushoto aliyekaa mstari wa mbele wakiwa katika Picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ruwasa na viongozi wa jumuiya ya watumia maji ya(NAMJI)inayosimamia mradi wa maji Nangomba-Mjimwema


Picha zote na Muhidin Amri

Na: Muhidin Amri,Nanyumbu

KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 Sahil Geraruma,ametembelea mradi wa maji safi na salama katika kijiji cha Nangomba uliojengwa na wakala wa usambazaji maji safi na usafi wa mazingira vijiji(Ruwasa)wilaya ya Nanyumbu.

Geraruma,amewapongeza Wahandisi na watendaji mbalimbali wa Ruwasa wilayani humo, kwa kutekeleza vyema ujenzi wa mradi huo wa maji ambao umetimiza lengo la Serikali la kumtua mama ndoo kichwani.

Geraruma ametoa pongezi hizo jana,mara baada ya kutembelea mradi huo umetekelezwa kwa lengo la kumaliza changamoto ya huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa vijiji viwili vya Nangomba na Mjimwema.

“Wahandisi wa Ruwasa nawapongeza sana kwa kuendelea kujenga na kusimamia mradi huu,mmefanya kazi nzuri sana,Serikali kupitia mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 inawapongeza”alisema.

Alisema, wataalam hao wameonyesa namna watendaji wa taasisi za umma wanavyotakiwa kutimiza wajibu wao katika kujenga na kusimamia miradi muhimu ya maendeleo katika jamii.

Amewataka kuendelea kuchapa kazi,kutanguliza uzalendo,kuwa makini na kuhakikisha miradi yote inayojengwa ina kuwa na ubora na viwango vinavyotakiwa.

Amewataka wataalam wa taasisi nyingine za umma katika mkoa wa Mtwara,kujifunza kwa Ruwasa namna miradi inavyojengwa pindi wanapopewa dhamana ya kutekeleza miradi ya maendeleo yenye lengo la kuwaondolea wananchi kero na kuharakisha maendeleo ya nchi.

Aidha,ameishukuru familia ya mkazi wa kijiji cha Nangomba Said Abdul kwa uzalendo wake kufuatia kutoa eneo lililojengwa mradi huo bure, na kumuagiza meneja wa Ruwasa wilaya ya Nanyumbu Mhandisi Simon Mchucha kupeleka huduma ya maji kwa familia hiyo bila gharama yoyote.

Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa wilayani Nanyumbu Simon Mchucha alisema,mradi huo umetekelezwa katika vijiji vya Nangomba na Mjimwema kata ya Nangomba kupitia program ya malipo kwa matokeo(PforR) kwa gharama ya Sh.196,430,118.06.

Alisema, chanzo cha mradi ni kisima kirefu chenye uwezo wa kuzalisha lita 6,000 kwa saa na unahudumia zaidi ya wananchi 5,151 katika vijiji vya Nagomba na Mjimwema.

Mchucha alieleza kuwa,ujenzi wa mradi huo umehusisha vituo 11 vya kuchotea maji,ukarabati wa tenki la lita 50,000 nyumba ya mitambo, nyumba ya mlinzi,ununuzi wa pampu na Jenereta na kaya 23 zimeunganishiwa huduma ya maji.

Alitaja mafanikio mengine ni ukusanyaji mapato yanayotokana na mauzo ya maji ambapo wastani kwa mwezi ni Sh.1,270,530 ambapo fedha zilizokusanywa tangu mradi ulipoanza kutoa huduma Mwezi Oktoba 2021 hadi Machi 2022 kufikia Sh.8,892,285.

Mhandisi Mchucha alisema,mradi huo unaendeshwa na wananchi kupitia Jumuiya ya watumia maji(NAMJI)ambapo chombo cha watoa huduma za maji ngazi ya jamii kimefanikiwa kutoa ajira kwa watu 15 kati yao wanaume 2 na wawanawake 13.
Kwa mujibu wake,Ruwasa kupitia vikao na mikutano yam aji inayofanyika sehemu mbalimbali inawahamasidha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye zoezi maalum la sensa ya watu na makazi itakayofanyika Mwezi Agosti Mwaka huu.

Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu Yahaya Mhata alisema,huo ni mradi mkubwa kutekelezwa na Ruwasa katika Jimbo la Nanyumbu na ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha ambazo zimefanikilisha kujengwa kwa mradi huo.

Amewaasa wanufaika na wananchi kwa jumla,kuhakikisha wanatunza na kulinda miundombinu ya mradi huo ili iweze kudumu kwa muda mrefu kwa faida ya vizazi vya sasa na vinavyokuja

Previous articleSOMA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRILI 17-2022
Next articleMAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO ASHIRIKI MISA TAKATIFU YA SIKUKUU YA PASAKA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here