Home LOCAL GARI ZA IT MARUFUKU KUSAFIRISHA ABIRIA: KAMANDA MUTAFUNGWA

GARI ZA IT MARUFUKU KUSAFIRISHA ABIRIA: KAMANDA MUTAFUNGWA

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Wilbroad Mutafungwa akizungumza wakati wa kufunga rasmi Programu ya Mahakama ya watoto iliyokuwa ikitoa elimu ya Usalama Barabarani kwa wanafunzi wa shule tisa za msingi katika Jiji la Dar es salam. Hafla ya kufunga Programu hiyo ilifanyika jana April 2,2022 katika viwanja vya shule ya msingi Kongowe Dar es Salaam.


Mkuu wa Wilaya yaTemeke Jokate Mwegelo akimkabidhi vyeti kwa shule zilizoshiriki katika programu ya mahakama ya watoto iliyokuwa ikitoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi tisa za serikali Jijini Dar es Salaam chini ya Shirika la AMEND kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi. Tukio hilo lilifanyika April 2, Mwaka huu.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha usalama barabarani Wilbroad Mutafungwa (wa pili kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Amend Simon Kalolo (wa kwanza kulia) kwa pamoja wakimkabidhi zawadi ya picha Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam Jokate Mwegelo (kushoto). Picha aliyokabidhiwa inaonesha tukio la Mkuu wa Wilaya huyo alipokuwa akifungua moja ya tukio lililohusu masuala ya usalama barabarani ndani ya Wilaya yake.Tukio la kukabidhiwa picha hiyo limefanyika jana April 2-2022 wakati wa kufungwa kwa programu ya mahakama ya watoto uliyokuwa ikitoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi tisa za serikali katika mkoa huo.
Mkurugenzi wa Shirika la Amend Simon Kalolo (kulia) akimkabidhi zawadi ya picha Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha usalama barabarani Wilbroad Mutafungwa (wa pili kushoto) wakati wa kutamatisha Programu maalum ya Mahakama ya watoto iiyokuwa ikitoa Elimu ya usalama Barabarani kwa wanafunzi wa Shule za Msingi za Serikali Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika jana April 2,2022 katika shule ya msingi Kongowe iliyopo Mzinga Jijini Dar es Salaam.

Maafisa wa Jeshi la Polisi kutka Kikosi cha usalama barabarani wakifanya maandalizi ya vyeti na zawadi mbalimbali kwaajili ya kukabidhiwa wanafunzi na shule zilizoshiriki kwenye Programu hiyo


Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake ya kufunga Programu hiyo iliyofanyika jana April 2,2022 katika shule la msingi ya Kongowe Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo (kushoto) na Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha usalama barabarani Wilbroad Mutafungwa (kulia) wakifurahia jambo kutoka kwa wanafunzi waliokuwa wakiimba wimbo maalum wa usalama barabarani katika hafla maalum ya kufunga rasmi programu hiyo iliyofanyika jana April 2,2022 Jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Shirika la AMEND Simon Kalolo akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake ya utangulizi kuelezea mwenendo mzima wa Programu yao ya Mahakama ya watoto waliyokuwa wakiitekeleza kwa kutoa elimu ya Usalama Barabarani kwa wanafunzi wa shule tisa za msingi za Serikali katika Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama barabarani.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Shirika la AMEND Simon Kalolo (kushoto) wataki wa kufungwa wa Programu hiyo katika viwanja vya shule ya msingi Kongowe Dar es es Salaam.
Moja wa dereva wa Daladala aliyekamatwa na kufikishwa katika mahakama ya wototo iliyokuwa ikifanyika katika viwanja vya shule ya msingi kongowe. Dereva huyo alikamatwa na Askari wa kikosi cha usalama barabarani na kufikishwa kwenye mahakama hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na wanafunziwa shule ya msingi wakiwemo wenye ulemavu wa kusikia.
Dereva wa daladala akitia saini kiapo cha kukiri makosa yake mara baada ya kusomewa makosa yake na kuyakubali.

Dereva wa Daladala akikiri makosa yake alipokuwa akisoma kiapo chake na kuahidi kufuata sheria za usalama barabarani anapokuwa Barabarani

Mtaalamu wa Lugha za Alama kutoka katika moja ya shule za Msingi zilizoshiriki programu hiyo akitoa msaada wa wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia (hawamo pichani) kuelezea matukio yaliyokuwa yakiendelea katika hafla hiyo.


Wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia wakifuatilia kwa ukaribu matukio yanayoendelea katika hafla hiyo kutoka kwa mkalimani wao wa alama ya lugha (hayumo pichani) wakati wa kufunga rasmi Programu hiyo Jijini Dar es Salaam. PICHA NA: HUGHES DUGILO
DAR ES SALAAM.

Kamamda wa Kikosi cha usalama Barabani ACP Wilbroad Mutafungwa amepiga marufuku magari yote yanayokwenda nje ya nchi maarufu IT kusafirisha abiria na kuwataka madereva wa magari hayo kuacha mara moja vitendo hivyo na kwamba jeshi la Polisi litachukua hatua kari za kisheria na halitokuwa na msamaha kwa watakaotiwa hatiani.
 
Kamanda Mutafungwa ameyasema hayo jana April 2,2022 wakati wa kufunga Programu maalum ya Mahakama ya Watoto iliyokuwa ikilenga kutoa elimu ya Usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi tisa za Serikali katika Jiji la Dar es Salaam na kusema kuwa zoezi linaanza mara moja na litakwenda sambamba na kuyakama magari yote ya mizigo yanayobeba abiria.
 
“Zoezi hili linaanza mara moja na hili litaambatana na kuyakamata magari yote ya mizigo yanayosafirisha abiria sambamba na ukaguzi wa magari ambayo hayana stika za nenda kwa usalama Barabarani” amesema  Kamanda Mutafungwa.
 
Amefafanua kuwa Sheria imeyataka magari ya IT kuwa na abiria mmoja tu na sivinginevyo na kwamba kumekuwepo na ukiukwaji mkubwa wa sheria hiyo kwa kuona magari hayo yamekuwa yakifanyakazi ya kusafirisha abiria na kuhatarisha usalama wa abiria hao. 

“Sheria inawataka kubeba abiria mmoja tu na si vinginevyo na hii  haishii kwenye magari ya IT tu bali hata magari yanayobeba magazeti nayo ni marufuku kubeba abiria.katika, hili hatutakuwa na utani, dereva na wamiliki lazima wafuate sheria za usalama barabarani” amesisitiza ACP Mutafungwa.

Aliongeza kuwa iwapo abiria anataka kusafiri anatakiwa kwenda kwenye Vituo vya mabasi ya abiria ili kupata usafiri wa uhakika na unaotambulika kwa mujibu wa sheria.“Nasisitiza ni  marufuku abiria kupanda gari ya mizigo,tutashukua hatua Kali.Tunakumbuka ajali ya gari iliyotokea Tanga watu watano walipoteza maisha na walikuwa wanasafiri na gari ya mizigo aina ya Fuso” Aliongeza.

Akizungumza programu ya Usalama Barabarani iliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kwa kushirikiana na Shirika la Amend Kamanda Mutafungwa amesema programu hiyo ni muendelezo wa kufikisha elimu ya Usalama Barabarani na kupitia programu hiyo Kuna madereva ambao watakuwa mabalozi wa wengine katika kuhamasisha kuzingatiwa kwa sheria za barabarani.

Kwa upande mgeni rasmi wakati wa kufunga programu hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam Jokate Mwegelo mbali ya kutoa shukrani kwa Shirika la Amend kwa kutoa mafunzo ya Usalama Barabarani kwa wanafunzi wa Shule za msingi ,amesema suala la ulasama barabarani ni jukumu la kila mwananchi na wote wanatakiwa kufuata sheria bila shuruti 

Amesema kwa mujibu wa takwimu za Jeshi hilo zinaonesha kuwa kwa kipindi Cha mwaka 2021 watu 1245 walipoteza maisha yao na wengine 2, 023 walijeruhiwa kutokana na ajali za barabarani.”Kati ya takwimu hizo wanafunzi 56 walipoteza maisha na wengine 65 walijeruhiwa.Ni wazi kuwa jitihada zaidi zinahitajika katika kupunguza ajali na kundi ambalo liko hatarini ni wanafunzi ambao Shule zao nyingi ziko barabafani.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuliomba Jeshi la Polisi kuangalia namna ya kufanya kuhakikisha wanafunzi hawakai muda mrefu kwenye vituo vya daladala kwani madereva wengi wa daladala hawawapikii na hivyo wanafunzi kuchelewa kurudi majumbani.”Angalieni namna ya kuweka utaratibu ili madereva wa daladala wasiache wanafunzi vituoni.”

Pia amewataka Wakala wa Barabara Tanzania ( TANROADS) na Wakala wa Barabara Vijijini ( TARURA) kuhakikisha barabara zinakuwa salama kwa watumiaji wote huku akisisitiza umuhimu wa kuwekwa kwa alama za barabarani yakiwemo maeneo ya shule.

Awali Mkurugenzi wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo akizungumzia programu ya Mahakama ya Watoto amesema lengo ni kuendelea kufikisha elimu ya Usalama barabarani kwa jamii ya Watanzani na wamekuwa wakitoa mafunzo hayo katika shule mbalimbali nchini.

Aidha amesema uchunguzi unaonesha kuwa maeneo ya mijini na yanayoendelea zaidi ya asilimia tatu ya Watoto wanajeruhiwa kwa ajali za barabarani kila mwaka na zaidi ya asilimia 90 ya Watoto wanaoathirika ni wanaotembea kwa miguu huku akisisitiza Shirika lao litaendelea kushirikiana na wadau wengine katika kuifikisha elimu ya usalama barabarani kwa Watanzania.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here