Home LOCAL DC ILALA AMEAGIZA WATENDAJI ILALA KUSHIRIKIANA NA JUMUIYA YA WAZAZI ILALA

DC ILALA AMEAGIZA WATENDAJI ILALA KUSHIRIKIANA NA JUMUIYA YA WAZAZI ILALA

 





NA: HERI SHAABAN (CCM ILALA)

MKUU wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija ameagiza  WATENDAJI wa Halmashauri ya Jiji wote kutoa ushirikiano na Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala katika Utekelezaji wa  majukumu yao ya kazi

Mkuu wa Wilaya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija alitoa tamko hilo  katika Kampeni ya Jumuiya ya Wazazi ya upandaji miti 5000 katika  uzinduzi uliofanyika  Shule ya Sekondari ya Jumuiya ya Wazazi Tabata Kimanga Wilaya ya Ilala.

“Kukua kwa CCM kwa ajili ya Jumuiya, Jumuiya ya Wazazi ina jukumu kubwa sana naagiza kwa Watendaji wa Kata na Mitaa wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa kazi zinazofanywa na Jumuiya ya Wazazi kwani Jumuiya ya Wazazi ni Mzizi wa Malezi ya Familia” alisema Ludigija.

Lugigija alisema malezi ya familia yananzia ngazi ya Kata na mitaa hivyo Jumuiya hiyo ina jukumu kubwa sana kushirikiana na Watendaji wa Serikali katika kufatilia Maendeleo ya watoto ikiwemo shule.

Aliwapongeza Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Ilala Mohamed Msophe na Katibu wake wameupiga mwingi katika uwandaji wa kampeni ya kupanda miti 5000 kuipendezesha Wilaya  llala ya kijani .

Alipongeza Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala na Kamati ya Utekelezaji kwa kumuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Samia Suluhu Hassan katika utunzaji wa Mazingira.

Aliwagiza viongozi waliopewa dhamana kusimamia utunzaji wa miti hiyo  Kwa ajili ya kuipendezesha Jiji letu .

Alisema mabadiliko ya tabia ya nchi yana athiri nchi yetu kwa kiasi kikubwa kutokana na uharibifu wa Mazingira mkaa ni zao la misitu na Dar es Salaam ni watumiaji wakubwa wa rasilimali ya misitu .

Aliwataka wananchi wa Wilaya ya Ilala kila kaya kupanda miti mitano ikiwemo ya matunda na kivuli

Akizungumzia kampeni ya wilaya ya ilala kila mwaka wanapanda miti milioni 1.5 .miti mbalimbali ya matunda ikiwemo ya  kuzuia momonyoko na miti ya vivuli

Mwenyekiti wa JUMUIYA ya wazazi Wilaya ya Ilala Mohamed Msophe alisema miti hiyo 5000

KAMPENI ya Ilala ya kijani itasambazwa kila kata miti 20 ,ngazi ya matawi miti 15, Wilaya ya Ilala ina matawi 265 ya Jumuiya ya wazazi.

Aliwataka viongozi wake wa Jumuiya kupanda miti hiyo Shuleni,katika vituo vya Afya na Ofisi za SERIKALI,  Kamati ya Utekelezaji wilaya itakuwa inafanya ziara kufatilia Maendeleo yake mpaka inakuwa.

Kwa  upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya  ya wazazi Tabata Kimanga Zayana Rashid alipongeza Viongozi wa Wilaya wa Jumuiya na serikali katika kufanikisha kampeni ya Ilala ya Kijani.

Zayana amewataka viongozi wa Jumuiya hiyo kusonga mbele katika kutekezaji wa majukumu yao ikiwemo upandaji miti Kwa ajili ya utunzaji Mazingira na kuimalisha Jumuiya vizuri

Mwishoo

Previous articleBUNGE LAPITISHA BAJETI YA OR – TAMISEMI YA TILIONI 8.8/-
Next articleSERIKALI YATANGAZA NAFASI ZA KAZI 17,412 KWA KADA ZA AFYA NA ELIMU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here