Home Uncategorized CEO WA SIMBA AFANYA KIKAO NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI AFRIKA KUSINI,...

CEO WA SIMBA AFANYA KIKAO NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI AFRIKA KUSINI, GAUDENCE MILANZI KUELEKEA PAMBANO DHIDI YA ORLANDO PIRATES

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Barbara Gonzalez amekutana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Mstaafu, Gaudance Milanzi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea mchezo wa mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Orlando Pirates siku ya Jumapili ya Aprili 24, 2022.

Katika hatua nyingine Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mohammed Mchengerwa, amewaondoa wasiwasi wapenzi WA soka nchini kuhusu usalama WA timu hiyo itakapokuwa Pretoria kuwakabili Orlando Pirates kwenye Michezo huo.

Serikali imechukua hatua zote stahili kuhakikisha wachezajinwa Simba wanakuwa salama nchini AFRIKA Kusini, Mimi mwenyewe nilipanga niambatane na timu Lakini kwa sababu za majukumu mengine ya kikazi nimemtumia msaidizi wangu, Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Singo kuambatana na timu.



LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here