Home LOCAL CCM TAWI LA MABIBO LAWANOA WATIA NIA

CCM TAWI LA MABIBO LAWANOA WATIA NIA

Katibu wa Tawi hilo ambaye anaemaliza muda wake Fatuma Ngunji akizungumza wakati wa Semina maalum aliyoiandaa kwaajili ya watia nia walijitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi katika Tawi hilo kuelekea uchaguzi unaofanyika Jumapili April 24,202.

Mlezi wa Chama hicho Kata ya Mabibo Nafi Habibu akizungumza alipokuwa akitoa mada kwa watia nia hao katika kikao hicho kilichofanyika kwenye Ofisi za CCM kata ya Mabibo leo April 23,2022.


Mwenyekiti wa Chama hicho Mohamed mbonde akizungumzia misingi ya Chama hicho na kuwataka watia nia hao kuifahamu na kuishika wakiwa kwenye majukumu yao


Mwenyekiti wa Chama hicho Mohamed mbonde (katikati) akiwa na viongozi wengine, Katibu wa Tawi hilo anaemaliza muda wake Fatuma Ngunji (kusho) pamoja na Mlezi wa Chama hicho Kata ya Mabibo Nafi Habibu (kulia) wakifuatilia michango iliyokuwa ikitolewa na wajumbe wa mkutano huo (hawamo pichani) mara baada ya kumaliza kuwasilisha mada kuelekea uchaguzi utakaofanyika kesho April 24,2022


Baadhi wa wajumbe wa Mkutano huo wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na wawezeshaji.

DAR ES SALAAM

CHAMA  cha Mapinduzi CCM Tawi la Mabibo mkoani Dar es Salaam kimewapiga msasa wanachama wake na wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea kwenye uchaguzi wa Mashina ambao unafanyika kesho April 24,2022.

Akizungumza mbele ya wanachama hao wa CCM Tawi la  Mabibo, Katibu wa Tawi hilo anamaliza muda wake Fatuma Ngunji amesema kwaza anamshukuru Mungu Kwani ameongeza Tawi kwa miaka kumi na amejenga umoja na mshikamano. 

Amesema kuwa katika kuelekea uchaguzi ngazi ya shina wao kama viongozi wameendesha semina hiyo kwa watia nia ili kuwajengea uwezo katika uongozi lakini pia kuwafanya kuwa  wamoja,  Upendo na mshikamano. 

“kama mnavyoona Ndugu zangu waandishi wa habari ndani ya Chama chetu hivi sasa kuna chaguzi mbalimbali zinaendelea na kesho  tunaaza ngazi ya shina baadae jumuiya na tunaendelea hivyo  hivyo lazima tuwapige msasa”amesema Ngunji

Kwa upande wake mlezi wa Chama hicho Kata ya Mabibo Nafi Habibu amesema kuwa katika Kata hiyo kuna matawi 11  hivyo wao kama wajumbe na sehemu ya viongozi wamekuwa wakitoa semina hiyo ili kuwafanya kuwa viongozi bora na wanaujuwa majukumu yao na kesho chaguzi zinaaza ngazi mashika. 

Amesema kuwapa semina watia nia kunawafanya kujua majukumu yao lakini pia kunatoa fursa wana CCM kuwa kitu kimoja kwa kupendana miongoni na kwamba  hivyo lazima washikamane. 

Naye Mwenyekiti wa Chama hicho  Mohamed mbonde amesema Chama cha Mapinduzi  CCM kina misingi yake hivyo  wamewaleta pamoja watia nia hao na kuwanoa kwa kutoa semina elekezi ili kujua misingi ya uongozi.

Chama hicho hivi sasa kimeaza chaguzi mbalimbali ndani ya chama na wameanzia ngazi ya mashina na baadae maeneo mengine na mwisho ngazi ya Taifa.

Mwisho

.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here