Home BUSINESS BENKI YA CRDB YAFUTARISHA WATEJA WAKE NA YATIMA, ZANZIBAR

BENKI YA CRDB YAFUTARISHA WATEJA WAKE NA YATIMA, ZANZIBAR

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid akiwakabidhi sehemu ya sadaka ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa Muwakilishi wa Kituo cha Wazee cha Barabani, Mzee Ali Hamad Juma, Unguja Zanzibar ikiwa ni sadaka iliyotolewa na Benki ya CRDB kwa baadhi ya vituo. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki baada ya hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateje wake wa Zanzibar. Katikati ni Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo.



Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid akiwakabidhi sehemu ya sadaka ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa wawakilishi wa Watoto wanaolelewa katika vituo vya Watoto Yatima vya Mazizini na Assalaam, Unguja Zanzibar ikiwa ni sadaka iliyotolewa na Benki ya CRDB kwa baadhi ya vituo. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki baada ya hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateje wake wa Zanzibar. Katikati ni Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo.


Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja, wadau wa benki, pamoja na vituo vya watoto yatima na wazee Zanzibar iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mao Zedong na kuhudhuriwa na zaidi ya watu 450.

Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja, wadau wa benki, pamoja na vituo vya watoto yatima na wazee Zanzibar iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mao Zedong na kuhudhuriwa na zaidi ya watu 450.







Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya CRDB Bw.Fredrick Nshekanabo akizungumza wakati wa hafla ya Futari Maalum ailiyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja wao wa Tawi la Zanzibar, iliyofanyika katika viwanja vya Mao Zedung Unguja Wilaya ya Mjini.

Wateja wa Benki ya CRDB Tawi la Zanzibar wakipata furati maalum walioandaliwa katika viwanja vya Mao Zedung Unguja Jijini Zanzibar.








Meneja Mwandamizi wa Al-Barakah Banking CRDB Bw.Muhsin Mohamed Said akizungumza na kutowa maelezo ya huduma ya Benki ya Kiislam ya Al-Barakah wakati wa hafla ya futari maalum iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja wa benki hiyo Tawi la Zanzibar niliyofanyika katika uwanja wa Mao Zedung Unguja Jijini Zanzibar.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana akizungumza na kutowa salamu kwa Wananchi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin kuzungumza katika hafla ya Futari Maalum ilioandaliwa Benki ya CRDB Tawi la Zanzibar kwa Wateja wao iliyofanyika katika uwanja wa Mao Zedung Unguja Jijini Zanzibar.

Mgeni rasmin Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zuberi Ali Maulid akizungumza na kutoa nasaha zake kwa Wananchi wakati wa hafla ya Futari Maalum iliyoandaliwa na Benki ya CRDB Tawi la Zanzibar kwa Wateja wao iliyofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung Unguja Jijini Zanzibar.


Meneja Kanda ya Mashariki wa Benki ya CRDB.Bw.Badru Iddi akizungumza na kutowa neno la shukrani kwa Wananchi na Wateja wa Benki ya CRDB Tawi la Zanzibar, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari maalum iliyowaandalia Wateja wao katika uwanja wa mao zedung Unguja Jijini Zanzibar.

Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi akisoma dua baada ya kumalizika kwa hafla ya Futari Maalum iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja wao Tawi la Zanzibar iliyofanyika katika uwanja wa Mao Zedung Unguja Jijini Zanzibar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here