Home LOCAL ASILIMIA 10 YA WATU WANAOISHI AFRIKA WANA UGONJWA SUGU WA FIGO

ASILIMIA 10 YA WATU WANAOISHI AFRIKA WANA UGONJWA SUGU WA FIGO


Mganga mkuu wa Serikali Dkt. Aifelo Sichalwe akifungua zawadi aliyokabidhiwa na muuguzi mkuu kitengo cha vyama vya wauguzi wa nefonolojia afrika Dkt. Divina Nyirera kutoka nchini Kenya.

Miongoni mwa washiriki wa kongamano la kisayansi la wauguzi wataalamu wa Figo kutoka nchi Tisa za Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu ikiongozwa na Mganga mkuu wa Serikali Dkt. Aifelo Sichalwe.

Na. WAF – Dar es Salaam 

Asilimia 10 ya watu duniani wanaishi na magonjwa sugu ya figo huku asilimia 50 ya watu wenye umri zaidi ya miaka 75 wana ugonjwa sugu wa Figo.

Hayo yamesemwa  na Mganga mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe wakati wa ufunguzi wa kongamano la kisayansi la wauguzi wataalamu wa Africa lililofanyika jijini  Dar es Salaam.

“Dhima ya kongamano hili ni kuleta maendeleo ya huduma ya magonjwa ya figo Duniani ambapo jukumu la elimu na ubunifu kwenye nchi za Afrika na dhima hii imekuja kwa wakati muafaka ambapo Tanzania inaenda kuimarisha na kupanua upatikanaji wa huduma za figo”. Amesema Dkt. Sichalwe.

Dkt. Sichalwe amebainisha kuwa  Mpaka Janauri 31, 2022 wagonjwa 2750 nchini Tanzania kwa sasa ndio wanapata huduma ya kusafishwa damu (dialysis) na kufikia tarehe 31 Januari mwaka huu wagonjwa 325 wamepandikizwa Figo. 


Pia, Kati yao wagonjwa 93 wamepandikizwa nchini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa 67 na Hospital ya Benjamin Mkapa Dodoma 26.

Aidha Dkt. Sichalwe amesema kwasasa hospitali zinazotoa huduma ya kusafisha damu nchini ni pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili, hospitali zote za Rufaa za Kanda (Bugando, KCMC, Benjamin Mkapa, Mbeya na muhimbili) na hospitali za Rufaa za Mikoa ya Kagera, Mwanza, Musoma, Kigoma, Arusha, Iringa na Mtwara.

“Ni matumaini yangu kuwa kongamano hili litatusaidia kujua hali halisi ya ugonja huu, changamoto tunazokutana nazo katika kutoa huduma za afya ya figo na njia za kuweza kukabiliana nayo”. Amesema Dkt. Sichalwe 

Hata hivyo Dkt. Sichalwe amesema Pamoja na kuimarisha huduma za magonjwa ya figo katika nchi zetu, Wauguzi lazima kujipanga kuweka jitihada za kipekee ili kupambana na ugonjwa huu hatari kwa kuimarisha afya za kinga kwa kuwa kinga ni bora kuliko tiba.

Kongamano hilo linafanyika kwa siku mbili ikiwa limehudhuriwa na idadi ya nchi tisa za Afrika ikiwepo nchi ya Kenya, Uganda, Misri, Rwanda, Sudani ya kusini, Burundi, Ghana, Zambia na wenyeji Tanzania.

Previous articleBENKI YA CRDB YASHINDA TUZO MBILI ZA MASUALA YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI KITAIFA DODOMA
Next articleMAKAMU WA RAIS AKISHIRIKI KUAGWA KWA MWAI KIBAKI KENYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here