Home SPORTS YAIFA STARS, SUDAN NGOMA DROO, ZATOKA 1-1 MECHI YA KIRAFIKI KWA MKAPA

YAIFA STARS, SUDAN NGOMA DROO, ZATOKA 1-1 MECHI YA KIRAFIKI KWA MKAPA

TANZANIA imeshindwa kutamba nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Sudan katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Sudan walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya pili likifungwa na Sadiq Totto baada ya kipa Metacha Mnata kuutema mpira hadi mapumziko wageni walienda wakiwa na bao hilo moja.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko na katika dakika ya 67 Simon Msuva aliisawazishia Taifa Stars akimalizia pasi ya George Mpole.

Mchezo huu ulikuwa wa pili kwa Tanzania baada ya mchezo wa kwanza kucheza na Afrika ya Kati na Stars kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Credit – Fullshangwe Blog

Previous articleTANZANIA NA ISRAEL KUSHIRIKIANA KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZA MAGONJWA YA MOYO KWA WATOTO
Next articleGHANA YAFUZU KUCHEZA KOMBE LA DUNIA QATAR 2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here