Home LOCAL WAZIRI UMMY AWATAKA WANAWAKE KUCHUNGUZA AFYA ZAO MARA KWA MARA

WAZIRI UMMY AWATAKA WANAWAKE KUCHUNGUZA AFYA ZAO MARA KWA MARA





 
Na: WAF – Dar es Salaam

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewataka wanawake kuchunguza Afya zao mara kwa mara ili kuwahi kupata matibabu endapo itabainika kuwa na ugonjwa.

Waziri Ummy amesema hayo jana wakati wa maadhimisho ya miaka 10 ya ubunifu wa mitindo wa mavazi ya Katty Collection yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam.

Waziri Ummy amebainisha kuwa katika kila wagonjwa mia moja (100) wanaoumwa saratani, wagonjwa 80 saratani imeshakua katika hali ya juu na matibabu kuwa magumu.

“Naomba nitumie jukwaa hili kuwahimiza wanawake kujenga utamaduni wa kujua Afya zetu mara kwa mara pamoja na kina baba pia.” Amesema Waziri Ummy.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amesema bado ugonjwa wa UVIKO-19 upo na kuwataka wananchi waendelea kujitokeza kupata chanjo kwa kuwa haina madhara kama baadhi ya watu wanavyosema.

Pia amesema kuna aina ya kirusi kipya kimeibuka nchini China, Japan pamoja na Korea hivyo amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari huku akisisitiza wananchi kujitokeza kupata chanjo.

“Kwa sasa kitu ambacho kinaweza kutusaidia kujikinga na UVIKO-19 ni chanjo kwa kuwa chanjo ni salama sana, nawaomba wote ambao hamjapata mkapate chanjo ili tuweze kujikinga”. Amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy katika kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Katty Collection za kuwainua wanawake kiuchumi ameweza kuchangia vyerehani 10.

“Wanawake tunyanyuane maana Ukimuwezesha mwanamke mmoja umewawezesha watu wengi waliokuwa nyuma yake.” Amesema Waziri Ummy

Previous articleTANZANIA NA KENYA ZAKAMILISHA ZOEZI LA UWEKAJI VIGINGI KUTATUA MIGOGORO YA KIMPAKA.
Next articleJESHI LA POLISI, SHIRIKA LA AMEND WAENDELEA KUTOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI HUKU WATOTO WA SHULE WAKITOA KIBANO KWA MADEREVA WAZEMBE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here