Home LOCAL WAZIRI NGWAJIMA AMEANDA TUZO KWA AJILI YA MTAA WA AMANI KIPUNGUNI.

WAZIRI NGWAJIMA AMEANDA TUZO KWA AJILI YA MTAA WA AMANI KIPUNGUNI.

NA: HERI SHAABAN, DAR
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Makundi Maalum Dkt, Dorothy Ngwajima,amesema MTAA wa AMANI Kata ya Kipunguni anaandaa tuzo Maalum kwa ajili ya Mtaa AMANI.

Waziri Dkt,Dorothy  Ngwajima alisema hayo katika ziara yake kukagua maenesho na kazi za Mikono  zinazofanywa na Sauti ya Jamii katika wiki ya madhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

“Ninawapongeza viongozi wa Mtaa wa Amani  kata ya Kipunguni ,Mtaa wa Amani ni Mtaa wa darasa la kujifunza kwa TANZANIA wamefanya kitu kikubwa kuanzisha SAUTI ya Jamii kumshughulikia maswala ya ukatili Wizara yangu itaweka kambi kujifunza pamoja na kuwapa tuzo ya Wizara kwa ubunifu wao” alisema Dkt , Ngwajima.

Dkt, Dorothy Ngwajima alisema atawaleta wataalam wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kurekodi dokomentary na kujifunza .

Aidha alisema Wenyeviti wa Serikali za mitaa ni chanzo cha Ustawi wa Jamii amewataka  wabuni vitu vya kupinga ukatili kwa ajili ya kusaidia Jamii kupinga vitendo hivyo.

Waziri Dkt, Ngwajima aliwataka wanaume kuunga mkono juhudi za Sauti ya Jamii Kipunguni 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija alisema maswala ya ukatili ya kijinsia Wananchi wa Wilaya ya Ilala wanapewa Elimu ya kutosha  matukio ya kijinsia.

Alisema yakitokea matukio hayo wanayapatia ufumbuzi wake kupitia madawati ya jinsia Wilaya ya Ilala.
.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kipunguni Daniel Malagashimba aliwataka Maafisa Ustawi wa Jamii washirikiane na Wenyeviti wa Serikali za mitaa  katika maswala ya ukatili wa kijinsia.

Malagashimba alisema Wenyeviti wa Serikali za mitaa wanateleleza Ilani ya chama Cha Mapinduzi CCM kwa ajili ya kuisaidia Serikali kutatua changamoto wanazofanyiwa Wana Jamii.
Mwisho.
herishaban@gmail.com

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here