Home LOCAL WATOTO KIGAMBONI WATOA KIBANO KWA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA MOTO WANAOKIUKA SHERIA...

WATOTO KIGAMBONI WATOA KIBANO KWA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA MOTO WANAOKIUKA SHERIA ZA BARABARANI

DAR ES SALAAM.

WATUMIAJI wa vyombo vya moto wilayani Kigamboni mkoani Dar es Salaam wamesema hawako tayari kuendelea kuvunja sheria za usalama barabarani baada ya kukiri mbele ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Maweni waliokuwa wakitoa hukumu kwa wavunja sheria hizo kupitia programu ya Mahakama ya Watoto.

Kupitia Mahakama ya Watoto inayotekelezwa na Jeshi la Polisi nchini Kikosi cha Usalama Barabarani kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la Amend walitoa mafunzo ya elimu ya salama barabarani kwa wanafunzi na baada ya mafunzo hayo wanafunzi hao  wamekuwa ‘Mahakimu’ wa kuendesha kesi na kutoa hukumu kwa madereva wavunjifu wa sheria za barabarani

Wakizungumza baada ya kufanyika kwa Mahakama ya Watoto iliyofanyika Shule ya Msingi Maweni Kigaomboni, baadhi ya madereva ambao walibainika kuvunja sheria kwa kutosimama eneo la wavuka kwa miguu kwenye barabara inayopita katika shule hiyo wamesema wamejisikia vibaya kuona wamekosea na kufundishwa na watoto kuhusu sheria za barabarani.

Mmoja ya madereva ambao wamujikuta wakiangukia kwenye Mahakama ya Watoto , Mansour Hilally pamoja na kupongeza ubunifu uliofanywa na Polisi kwa kushirikiana na Shirika la Amend kwa upande wake amejisikia vibaya kuwekwa kiti moto na wanafunzi ambao kwake ni watoto wake , hivyo ameahidi kutovunja tena sheria za usalama barabarani.

“Ni kweli nilivunja sheria ya usalama barabarani, nilipofika eneo kwenye kivuko cha wenda kwa miguu eneo la shule hiyo sikusimama,hivyo nikasimamishwa na Trafiki na baada ya hapo nikapelekwa kwa wanafunzi waliokuwa katika chumba maalum, nikaelezwa kosa langu.

“Nimepata somo kubwa sana kusemwa na watoto kuwa umekosea ni aibu sana, tumeshaozea kuchukuliwa hatua na matrafiki na hao tumeshawazoea , lakini leo nimejikuta mbele ya wanafunzi, kwa kweli sitarudia tena kuvunja sheria za barabarani, Salehe Zahoro

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Polisi ambaye pia ni Ofisa Operesheni wa Usalama Barabarani Adam Maro amesema jeshi lao kwa kushirkiana na Amend wamesimamia kufanyika kwa Mahakama ya Watoto na lengo kuu ni kuwambusha watumiaji vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabara  ili kuepuka kusababisha vifo na ulemavu wa kudumu.

“Wakati Mahakama ya Watoto ikiendelea wote ambao wamevunja sheria za usalama barabarani na kufikshwa mbele ya wanafunzi waliokuwa wakiwasikiliza madereva hao wamekiri kuwa wamekosea na jambo la kufurahisha wamesema hawatarudia tena na watakuwa mabalozi wa wengine kuwakumbusha kuzingatia sheria zilizoo kueuka ajali zisizokuwa za ulazima.

“Kupitia wanafunzi hawa ambao wameendesha Mahakama ya Watoto kwa kujiamini na kutoa maelezo yaliyonyooka inaleta ishara kwamba huko mbele ya safari haitakuwa vigumu kuwapata Polisi ambao watakuwa kwenye kikosi cha usalama barabarani.Wanafunzi hawa watakuwa mabalozi katika kufikisha elimu hii na tunatamani iwe endelevu,”amesema Kamishna Msaidizi wa Polisi Maro.

Wakati huo huo Mkurugenzi  wa Shirika la Amend Simon Kalolo amesema wao kwa kushirikiana na Polisi  kikosi cha usalama wa barabarani  wamekuwa na Mahakama ya Watoto na wameamua kuwatumia wanafunzi hao kwa kutambua wao ndio wahanga wakubwa wa ajali za barabarani.

Amesema madereva karibia wote ambao wamefikishwa mbele ya mahakama hiyo wameonesha kuguswa na makosa waliyoyafanya na kujikita wakiwa mbele ya wanafunzi hao ambao wamepatiwa elimu ya kutosha kuhusu elimu ya usalama barabarani.”Wanafunzi hawa wameonesha umahiri mkubwa wa kuuliza maswali kwa wavunjifu wa sheria hizo.”

Kuhusu mradi huo Kalolo amesema mradi wa Mahakama ya Watoto umefanyika katika shule nane za Serikali katika Mkoa wa Dar es Salaam na imewafikia wanafunzi wote wakiwemo wenye mahitaji maalum ambao nao wamekuwa wahanga wa ajali za barabarani.”Mradi huu utakuwa endelevu kwa maeneo mengine kwani tunataka kuwafikia watumiaji wengi wa barabara hasa watumiaji wa vyombo vya moto, tunafahamu Serikali imekuwa imara katika kusimamia sheria hizo na sisi tunayo nafasi ya kusaidia katika kupunguza ajali za barabarani kwa kutoa elimu kwa wananchi hasa wanafunzi.”

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha usalama barabrani Makaao Makuu  AS  Mossi Ndozero  amewakumbusha madereva wa daladala mbali ya kuzingatia sheria wahakikishe wanakuwa nadhifu wakati wote hasa kwa kutambua wamekuwa wakibeba wato wa kada mbalimbali .

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here