Home LOCAL WANAWAKE WA MKOA WA DODOMA WACHANGA TSH: Mil. 17 NA KUWAPATIA TAASISI...

WANAWAKE WA MKOA WA DODOMA WACHANGA TSH: Mil. 17 NA KUWAPATIA TAASISI YA JAI

Na: WAF – CHEMBA.

Wanawake wa Mkoa wa Dodoma wachanga kiasi cha Tsh. mil 17 ambapo kiasi cha fedha taslimu Tsh. Mil. 6 na ahadi ni Tsh: 11, taulo za kike pamoja na vyakula na kuwakabidhi taasisi ya jumuiya ya kiislami (JAI)

Harambee hiyo imefanyika leo machi 8, 2022 ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka kwenye maadhimisho ya sherehe za wanawake zilizofanyika katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.

Mhe. Mtaka amefanya harambee hiyo baada ya kujua shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo ikiongozwa na wanawake wengi kwa kusaidia wagonjwa wasiokuwa na uwezo wa vyakula, dawa na hata matibabu.

Aidha,Mkuu wa Mkoa Mhe. Mtaka amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Corona kwa hatua zote zinazotolewa na wataalamu wa Afya ikiwemo kuvaa barakoa na kunawa mikono.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Bi. Neema Majule amewashauri wanawake kuwa viongozi katika kuwaelimisha na kuwahamasisha wengine kujitokeza kuhesabiwa kwenye Sensa ya watu na makazi. 

Pia, amewasihi wanawake kuungana kwa kufanya miradi mkubwa wa maendeleo hapo wataonesha mabadiliko na kuweza kujikomboa kichumi.

“Kila mwanamke ajitahidi kujikwamua kiuchumi, huo ndio wito wangu kwa wanawake siku ya leo”. Amesema Bi. Majule

Naye, mkuu wa wilaya ya Chemba mkoani Dodoma mhe. Simon Chacha ambae ndio mwenyeji wa shughuli hiyo amewasihi wanawake kuwa na malezi mazuri kwa watoto wao bila kuwaachia Wasaidizi wa ndani pekee.


“Leo ni siku yenu wanawake, mkawe na malezi mazuri kwa kuwa mwanamke akifanikiwa basi mwanaume anafanikiwa zaidi”. Amesema Mhe. Chacha 

Vile vile, Mtoa risala Bi. Mary Barnabas ambaye pia ni kaimu mwenyekiti wa jukwaa la wanawake uwezeshaji kiuchumi Mkoa wa Dodoma ameishukuru Serikali kwa kuwawezesha wanawake kupata mikopo na kuteuliwa katika nafasi mbalimbali katika uongozi. 

“Tumeona viongozi wengi katika nafasi kubwa na ndogo kama kiongozi wa nchi Rais ni mwanamke, waziri wa Afya ni mwanamke, waziri wa ulinzi ni mwanamke na wakuu wa Mikoa/Wilaya pia wapo“. Amesema.

Sherehe hizo ambazo zimezinduliwa rasmi mwaka 1911 hadi leo ni zaidi ya miaka 100 ambapo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka katika Mkoa wa Dodoma wakiwemo viongozi wa wizara ya Afya na wizara nyingine ambazo hufanyika kila tarehe 8 ya mwezi wa tatu.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here