Home BUSINESS WAJASIRIAMALI WA ZAO LA MCHIKICHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO KIGOMA

WAJASIRIAMALI WA ZAO LA MCHIKICHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO KIGOMA

Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Kigoma  Bw. Gervas Ntahamba ametoa wito kwa Wajasiriamali wanaojishughulisha na zao la mchikichi mkoani humo kichangamkie fursa ya kuanzisha viwanda vidogo vya ukamuaji wa mafuta ya mchikichi kwa kuwa Serikali imedhamilia kwa dhati kuinua  kilimo cha zao la mchikichi  katika jitihada za kuondoa upungufu wa mafuta ya kula nchini. 

Ameyasema hayo wakati akitoa mafunzo ya awali ya Mradi wa Kiwanda cha kisasa cha kuchakata mazao ya mchikichi  kwa wajasiliamali wa kikundi cha Tukazanie Maandeleo cha Kijiji cha Sunuka Wilaya ya Uvinza Machi 15, 2022 yaliyoandaliwa na Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) – Enhanced Intergrated Framework (EIF) 

Aidha, Bw. Ntahamba amewashauri wajasiriamali wa mkoa huo kupata mafunzo stahiki katika mnyororo wa thamani  wa zao la mchikichi kupitia  SIDO ili wapate ujuzi na uwezo wa kuchakata mafuta ya mawese, mise na bidhaa nyingine zinazotokana na  zao la chikichi kwa ubora, tija na ufanisi  kwa kutumia teknolojia ya kisasà na rafiki.

Bw. Ntahamba pia amesema mafunzo hayo ya awali ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi EIF  katika ujenzi wa viwanda viwili vidogo vya kuchakata mafuta na bidhaa zinazotokana na zao la chikichi ambapo  kiwanda kimoja kitakuwa na  mashine ya kukamua mafuta ya mawese lita  takribani 2000 kwa siku, Mashine ya kukamua mafuta ya mise lita 80 kwa saa, Mashine ya kubangua mise tani moja kwa saa na vifaa mbalimbali vya kutengeneza bidhaa hizo. 

Naye, Bi Ritta Magere Mratibu na Msimamizi wa Mradi wa EIF Tier I na II kutoka Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara amesema  mafunzo hayo yamelenga kuwaelimisha wajasiliamali hao kuhusu uchakataji na usindikaji wa mazao yatokanayo mnyororo wa thamani wa zao la  chikichi ili kukuza uwekezaji na mauzo kwenye masoko ya ndani kikanda na kimataifa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo kwa Mkoa wa Kigoma. 

Nao Washiriki wa mafunzo hayo walioata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali yanayolenga kuboresha uelewa wao katika kuhusu hatua sahihi za kufuata katika  uchakataji wa mafuta ya maweze, mafuta ya mise na bidhaa zinazotokana na zao la chikichi kwa ubora  tija na ufanisi ili kuongeza ajira na kipato katika familia zao na taifa kwa ujumla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here