Home BUSINESS UONGOZI BARRICK WATOA NENO KUHUSU UCHAFUZI WA MAJI MTO MARA, WASEMA HAWAHUSIKI

UONGOZI BARRICK WATOA NENO KUHUSU UCHAFUZI WA MAJI MTO MARA, WASEMA HAWAHUSIKI

Na: Mwandshi Wetu.

UONGOZI wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara inaomikikiwa Kwa pamoja na Kampuni ya Barrick na Serikali ya Tanzania umesema auhusiki na uchafuzi wa maji ya mto Mara.

Taarifa iliyotolewa na Kampuni hiyo leo Jana kufuatia taarifa za kuwepo na uchafuzi wa maji katika mto ikihusisha kemikali ya Zebaki, imesema mbali na mgodi huo kuwa umbali zaidi ya kilometa 85 pia Zebaki si sehemu ya orodha ya vitendanishi vya mgodi huo hivyo basi Zebaki inayohisiwa kuwemo mto Mara haitoki kwenye mgodi huo.

Meneja wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa amesema Mamlaka ya Bonde la Maji ya Ziwa Victoria mara kwa mara Imekuwa kichukua sampuli za maji katika maeneo yaliyo jirani na migodi na mgodi wenyewe una mpango madhubuti wa ufuatiliaji wa maji ya ardhini  na hakuna ushahidi wa kuwepo zebaki au uchafu mwingine wowote kwenye maji ndani au karibu na maeneo ya uzalishaji.

“Serikali ya Tanzania iliunda timu ya wataalamu inayoongozwa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambayo imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara ili kuhakikisha hakuna uchafuzi wa mazingira au maji unaotokea katika mgodi huo na katika maeneo yanayouzunguka,” amesema Georgia kwenye taarifa hiyo.

Aidha amesema Mgodi pia umefikia lengo muhimu la uhifadhi wa taka zitokanazo a mchakato wa uchenjuaji wa madini kwa kupunguza kiasi cha maji yaliyohifadhiwa kwa kiasi kikubwa kutoka mita za ujazo milioni 7 hadi mita za ujazo 800,000 ndani ya kipindi cha miaka miwili, kama ilivyokubaliwa katika Mkataba wa Maelewano na NEMC. 

Amesema hayo ni mafanikio makubwa, ambayo yanaonyesha zaidi dhamira na jitihada za Mgodi wa Dhahabu wa North Mara zinakwenda sambamba kwa kuhakikisha hakuna uchafuzi wa maji au mazingira kwenye Mgodi na maeneo yanayouzunguka.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here