Home LOCAL UMOJA WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII TANZANIA WAPONGEZWA KWA KUENDELEZA KUTOA...

UMOJA WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII TANZANIA WAPONGEZWA KWA KUENDELEZA KUTOA HUDUMA BORA KWA JAMII

 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameupongeza Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania kwa kuanzia umoja huo kwa lengo la kuendeleza kutoa huduma bora kwa Jamii.

Mhe. Hemed ameeleza hayo Ofisini kwake Vuga alipokutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Umoja huo kwa lengo la kupata maelekezo kutoka kwake juu ya uboreshaji wa huduma zao.

Mhe Hemed amesema ni jambo la kupongezwa kwa kufikiria kuanzisha umoja huo wakiwa na lengo la kuzidisha ushirikiano na kuwataka kujikita zaidi katika mambo yatakayosaidia kukuza uchumi wa Tanzania.

Makamu wa pili wa rais amesema amefarijika sana kuona umoja huo unaandaa mafunzo mbali mbali ya kiutendaji ili kuhakikisha wanakuza uzoefu baina yao na kueleza kuwa uzoefu huo utaimarisha Huduma za Kijamii.

Aidha Mhe. Hemed amewaeleza wajumbe hao kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina malengo mengi ya kukuza uwekezaji kupitia Taasisi mbali mbali za Kijamii ikiwemo Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iliopo nchini kwa lengo la kuwekeza miradi mbali mbali ya maendeleo.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi hao Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF)Bwana Mussa Ibrahim Iyombe amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa umoja huo umefarijika kwa Nia Njema ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuthamini juhudi zinazofanywa na Mifuko ya hifadhi ya Jamii Tanzania na kumuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina yao kwa Maslahi ya Taifa.

Aidha Bwana Iyombe amemuhakikisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania Bara wataangalia namna bora ya kuja kuwekeza Zanzibar kwa kufata taratibu salama.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
03 Machi 2022

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here