Na: Costantine James, Geita.
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Geita Zahara Michuzi amesema ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu unaojengwa eneo la magogo ndani ya halmashauri hiyo umefikia asilimia 65% mpaka hivi sasa.
Amesema hayo wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya mkoa wa Geita ya kukagua miradi mbali mbali ya kimaendeleo ndani ya halmashauri ya Geita mji iliyoongozwa na mjumbe wa halmashauri kuu ya Ccm Taifa Evarist Gervas katika kukagua utekeleza wamiradi ya kimaendeleo iliyotekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja chini Rais Samia Suluhu Hassani tangu alipoingia madarakani hadi sasa.
Zahara amesema ujenzi wa uwanja huo mpaka sasa umefikia asilimia 65% huku akisema mpaka kufikia mwezi may 2022 utakuwa umekamilika kwa awamu ya kwanza ili uanze kutumika kama ulivyokusudiwa.
Amesema kukamilika kwa ujenzi wa uwanja huo utaongeza chachu ya shughuli za kimaendeleo kwani utakapo kamilika watu wengi watapata fursa ya kufanya biasharambali mbali hivyo kuchangia ongezeko la mapato katika serikali.
Aidha Zahara amesema wanaendelea kujituma zaidi ili ujenzi wa uwanja huo ukamilike kama ulivyopangwa kwa lengo la kutekeleza timu ya Geita Gold Fc kuwa na uwanja wake hali itakayowezesha mashabiki watimu hiyo kushudia mechi mbalimbali katika dimbahilo.
Awali Mhandisi Oswald C. Mtei wakati akisoma taarifa ya ujenzi wa uwanja huo kwa kamati ya siasa ya mkoa kwa niaba ya mkurugenzi alisem a ujezi wa uwanja wa magogo unaendelea na uko katika hatu mbali mbali katika katika maeneo tofauti kama ujenzi wa ukuta,mtaro wa maji ya mvua pamoja na jukwaa kuu.
Mhandisi Oswald alisema ujenzi wa utayarishaji wa sehemu ya kuchezea (pitch) umekamilika hatua inayofuata ni uwekaji wa mabomba ya maji chini ya ardhi, udongo, mbolea na kasha kuotesha majani.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya Ccm Taifa ndugu Evarist Gervas alisema kamati ya siasa imelizishwa na mwenendo wa ujenzi wa uwanja huo ulipofikia.
Gervas akatumia nafasi hiyo kumtaka mkurugenzi wa halmashauri ya mji Geita kusimamia kikamilifu ujenzi wa uwanja huo ili ukamilike kwa wakati uliopangwa hali itakayowezesha timu ya Geita Gold Fc kutumia uwanja huo katika michezo yake kama uwanja wa nyumbani.