Home Uncategorized TMDA KUTOA TUZO KWA WAANDISHI WA HABARI ZINAZOHUSU UDHIBITI WA DAWA, VIFAA...

TMDA KUTOA TUZO KWA WAANDISHI WA HABARI ZINAZOHUSU UDHIBITI WA DAWA, VIFAA TIBA NA BIDHAA ZA TUMBAKU

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imeandaa tuzo maalumu kwa  kazi za Waandishi wa Habari juu ya Udhibiti wa Dawa, Vifaa tiba, Vitenganishi na bidhaa za tumbaku kwa mwaka 2021-2022.

Kwa mujibu wa taarifa ya TMDA, tuzo hizo ni kwa Waandishi wa Habari ambao wameripoti taarifa na kuandaa makala mbalimbali kuhusu kazi na majukumu ya TMDA katika kipindi cha kuanzia Juni 2021hadi Februari  mwaka huu.

“Lengo ya tuzo hizo ni kutambua mchango wa Waandishi wa Habari na kuleta hamasa katika kuelimisha jamii kuhusu masuala ya udhibiti wa dawa, vifaa tiba, vitendanishi na bidhaa za tumbaku kupitia vyombo vya habari ili kulinda afya za jamii.” Ilieleza taarifa hiyo ya TMDA

Aidha, imebainisha kuwa, kazi zinazolengwa ni zile zilizoripotiwa kupitia Televisheni (TV), Redio, Magazeti na mitandao ya Kijamii kipindi hicho cha Juni 2021 hadi Februari mwaka huu.

“Kazi baada ya kupokelewa zitashindanishwa na hatimaye kuwapata washindi watakaopewa tuzo.

TMDA inawaalika Waandishi kuwasilishwa kazi zao ifikapo au kabla ya tarehe 30 Machi mwaka huu kupitia barua pepe ya:

tmda.award2022@gmail.com au kuwasilisha kazi kwa njia ya CD katika ofisi za TMDA zilizopo Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma, Mtwara, Tabora na Geita”. Ilimalizia taarifa hiyo.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here