Home LOCAL TANZANIA NA KENYA ZAKAMILISHA ZOEZI LA UWEKAJI VIGINGI KUTATUA MIGOGORO YA KIMPAKA.

TANZANIA NA KENYA ZAKAMILISHA ZOEZI LA UWEKAJI VIGINGI KUTATUA MIGOGORO YA KIMPAKA.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani akiwa juu ya moja ya Vigingi vya mpaka wa Tanzania na Kenya vilivyowekwa katika mbuga ya Serengeti mkoani Mara


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii katika mpaka wa Tanzania na Kenya ndani ya mbunga ya Serengeti mkoani Mara.


Moja ya Vigingi vya mpaka wa Tanzania na Kenya vilivyowekwa katika mbuga ya Serengeti mkoani Mara ili kumaliza mgogoro wa mpaka uliokuwepo hususani katika sekta ya utalii kati ya nchi zote mbili

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii wakiimba wimbo wa kumpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza Mwaka mmoja wa uongozi wake wakati wakiwa katika mpaka wa Tanzania na Kenya.

Picha zote na Hassan Mabuye

Na Anthony Ishengoma

Serikali ya Tanzania na Kenya zimekamilisha zoezi la uwekaji vigingi katika mpaka unaoigawa Tanzania na Nchi jilani ya Kenya katika mbuga ya Serengeti na hivyo kufanikiwa kumaliza mgogoro wa mpaka uliokuwepo hususani katika sekta ya utalii kati ya nchi zote mbili.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete alisema hayo jana wakati yeye na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili na Utalii walipofika katika Mbuga ya Serengeti kujionea utekelezaji huo unaosimamiwa na Wizara ya Ardhi.

Naibu Waziri Kikwete alisema zoezi la uwekaji vigingi katika mpaka huo wenye zaidi ya Km 60 utaiwezesha Serikali kupata mapato na sifa ambayo mbuga ya Serengeti iko nayo, akiongeza kuwa vingi hivyo vimewekwa karibu zaidi tofauti na awali ambapo vingingi hivyo viliwekwa kwa umbali mkubwa na kuwa ngumu zaidi kuvitambua.

‘’Katika kipindi cha mwaka mmoja Serikali ya Rais Samia na ile ya Kenya ziliweza kuingia katika makubaliano ambayo matokeo yake yamewezesha kutatua mgogoro uliokuwepo katika mpaka ndani ya mbuga ya Serengeti na kuleta heshima kubwa kwa nchi zote mbili.

Naibu Waziri huyo alitumia fursa hiyo kupongeza mafanikio ya Serikali kwa kipindi cha mwaka mmoja nakubainisha kuwa zoezi kama hilo pia litaendelea kati ya mipaka ya nchi nyingine jilani ikiwemo Uganda, Malawi na Kongo hasa katika mipaka iliyo ndani ya maji.

Naye Mwanyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Ally Makoa amewaagiza watendaji wa Wizara kuhakikisha wanatekeleza zoezi hilo na kuharakisha uweka  vingingi  katika mpaka, ili  kuondokana  na adha iliyopo katika utambuzi wa mipaka inayoigawa Tanzania na chi jilani.

“kazi hii iliyofanyika ni kazi nzuri sana na tunatamani sasa maeneo yetu yote yaliyohifadhiwa yawe na vigingi vya mipaka vinayoonekana kwa malengo yaleyale tuliyoyafanya hapa katika maeneo yote ya nje na ndani ya nchi kuwe na vigingi vivyoonekana ili pasiwe na uvamizi”. Makoa aliongeza.

Wizara ya ardhi itaendelea kutekeleza maelekezo ya Serikali na yale ya kibajeti na kutoa kipaumbele katika utatuzi wa migogoro baina ya Nchi jilani kwa kuweka vingingi katika mipaka ambavyo awali viliwekwa na wakoloni katika umbali mrefu na kusababisha sintofahamu katika baadhi ya maeneo.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii imehitimisha ziara ya kikazi kwa kutembelea program mbalimbali zinazotekelezwa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi baada kufuatilia utekelezaji wa  miradi hiyo katika Mkoa wa Singida, Mwanza na Mara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here