Home SPORTS SIMBA SC YAICHAPA RS BERKANE 1-0 KWA MKAPA

SIMBA SC YAICHAPA RS BERKANE 1-0 KWA MKAPA

Na: Stella Kessy, DAR.

Wekundu wa msimbazi Simba SC leo imeendeleza ubabe wa ushindi katika Dimba la nyumbani kwa kuichapa timu ya RS Berkshire ya Morocco goli 1-0 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Africa.

TImu ya Simba ilishuka Dimbani ikiwa na majeraha ya kufungwa ugenini na timu hiyo magoli 2-0 na hivyo kucheza kwa nguvu kwa kulishambulia lango la wapinzani wao mara kwa mara.

Dakika ya 44 kipindi cha kwanza Simba ilifanikiwa kupata bao la kuongeza kwa shuti Kali lililopigwa na Othman Pape Sakho na kuamsha shangwe za Mashariki wao zaidi ya elfu 30 waliokuwa wakishuhudia mchezo huo.

Mpaka dakika 90 zinamalizika timu hiyo ya wekundu wa msimbazi imeondoka na alama 3: muhimu kwa ushindi wa goli moja na kurudi kileleni mwa kundi D wakiwa na alama 7.


Previous articleWAKUU WA VITENGO VYA MANUNUZI NA UGAVI 23 WASHUSHWA CHEO
Next articleLETSHEGO AFRICA PRESS RELEASE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here