Home LOCAL SHILINGI BILIONI 2 KUMALIZA KERO YA MAJI MKONGO NA MASUGURU

SHILINGI BILIONI 2 KUMALIZA KERO YA MAJI MKONGO NA MASUGURU

Fundi sanifu wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira(Ruwasa)wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Salum Nachundu kushoto,akimtwisha ndoo ya maji mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Mkongo Zakia Simkala,baada ya Ruwasa kufikisha huduma ya maji kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi na walimu wa shule hiyo.


Tenki la maji lenye uwezo wa kuchukua takribani lita 100 linaloendelea kujengwa katika mradi wa maji kijiji cha Masuguru wilayani Namtumbo na Wakala wa usambazaji maji safi na usafi wa mazingira( Ruwasa) ambalo litakapokamilika litahudumia wakazi wapatao 3264 wa kijiji hicho.


Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mkongo wilayani Namtumbo wakichota maji katika kituo kimojawapo kilichojengwa na wakala wa usambazaji maji safi na usafi wa mazingira kupitia mradi mkubwa wa maji uliotekelezwa na Serikali kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa kijiji cha Mkongo na Nahimba.

Na: Muhidin Amri,Namtumbo

WIZARA ya maji kupitia wakala wa  maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,imeanza kutekeleza miradi ya maji katika vijiji mbalimbali ambavyo  kwa muda mrefu havikuwa na huduma hiyo.

Kaimu Meneja wa Ruwasa wilaya ya Namtumbo Salum Nachundu, alitaja miradi hiyo ni pamoja na mradi wa maji Mkongo Gulioni-Nahimba uliotekelezwa chini ya Programu ya maendeleo ya sekta ya maji(WSDP)kupitia program ndogo ya maji na usafi wa mazingira vijijini(RWSSP).

Alisema, mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2017na mkandarasi Kipera Contractors ambaye alitakiwa kukamilika kazi mwaka 2020,lakini alishindwa kukamilisha kazi kutokana na changamoto mbalimbali ikiwamo uwezo mdogo wa kiufundi na fedha.

Nachundu alieleza kuwa,baada ya Serikali kukatisha mkataba na mkandarasi, mradi huo umekamilishwa na wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa) kwa njia ya force akaunti ambapo kwa sasa umekamilika  na wananchi wanapata huduma.

Kwa mujibu wa Nachundu,mradi wa Mkongo gulioni-Nahimba ulisanifiwa kuhudumia wakazi 8,007  katika vijiji hivyo  ambapo awali gharama ya mradi ilikuwa Sh.2,069,975,521,hata hivyo zilipungua hadi Sh.1,451,531,411 baada ya Ruwasa kutekeleza mradi huo kwa kuwatumia mafundi wa kawaida.

Aidha, alitaja mradi mwingine  unaotekelezwa ni katika kijiji cha Masuguru ambao  unatarajia kuhudumia wananchi wapatao 3,264  na gharama za mradi huo ni Sh.402,000,000.

Kwa upande wake msimamizi wa mradi huo Gloria Nziku alisema,mradi wa maji katika kijiji cha Msuguru unatekelezwa chini ya program ya malipo kwa matokeo na ulianza kutekelezwa mwezi Agosti mwaka 2021 na unatarajia kukamilika tarehe 30 mwezi huu.

Nziku,ameishukuru wizara ya maji kutoa fedha na serikali ya kijiji na wananchi,kwa ushirikiano mkubwa  waliotoa wakati wa utekelezaji wa mradi huo ambao hadi sasa umefikia asilimia 85.

Alisema,mradi utakapokamilika jumuiya ya watumia maji Masuguru ndiyo watakuwa wasimamizi wakuu na waendeshaji wa mradi huo.
Amewataka viongozi wa jumuiya na wananchi kuhakikisha wanalinda miundombinu ya  mradi ili uendelea kufanya kazi kama ilivyokusudiwa na serikali.

Mkazi wa kijiji hicho Dolfina Chowo alisema,wanachangamoto kubwa yam aji safi na salama ambapo wanatumia maji ya visima vya kupampu na wakati mwingine maji ya visima na mito iliyopo kando ya kijiji hicho.

Alisema, sasa wana matumaini makubwa ya kuondokana na  kero hiyo baada ya serikali kupitia wakala wa maji safi na usafi wa mazingira(Ruwasa)kuanza kutekeleza mradi wa maji ya bomba ambao umeanza kuleta matumaini makubwa kwao.

Previous articlePROFESA NDALICHAKO AMEKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MWAKILISHI MKAZI WA UNFPA PAMOJA NA UGENI KUTOKA UNICEF
Next articleRAIS SAMIA AONGOZA WATANZANIA KATIKA KUMBUKIZI YA HAYATI DKT. MAGUFULI CHATO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here