Home LOCAL RIDHIWANI KIKWETE AWAHAKIKISHIA WATANZANIA SERIKALI KUTATUA MIGOGORO YA ARD

RIDHIWANI KIKWETE AWAHAKIKISHIA WATANZANIA SERIKALI KUTATUA MIGOGORO YA ARD

Na: Mwandishi Wetu.

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete amewahakikishia Watanzania kuwa Serikali imejipanga kutatua migogoro ya ardhi ikiwemo ile ya mipaka ya Wakulima na wafugaji.

Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema hayo mapema Machi 15,2022 wakatj akishiriki uzinduzi wa Wiki ya Maji Simanjiro Mkoani Manyara ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.

Akitoa salamu za Wizara ya Ardhi, Mhe Ridhiwani Kikwete amempongeza na kumshukuru Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga bajeti itakayowezesha utekelezaji wa majukumu ikiwemo kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji, mipaka baina ya Wilaya, Mikoa na Hifadhi na Usalama wa Ardhi.

“Wizara ya Ardhi imejipanga kuleta amani na utulivu kwa kutatua changamoto kwenye mipaka ya ardhi.” Alisema Mhe. Ridhiwani Kikwete.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here