Home SPORTS PABLO AELEKEZA NGUVU ZOTE LIGI KUU

PABLO AELEKEZA NGUVU ZOTE LIGI KUU

 

Na: Stella KESSY

KOCHA Mkuu wa klabu ya Simba Pablo Franco amesema kuwa baada ya timu kurejea kutoka kwenye mashindano ya kombe la Shirikisho Afrika sasa nguvu zote wanazielekeza katika ligi kuu ya NBC.

Pablo amesema kuwa kikosi chake kwa sasa wanamichezo miwili ya ligi inayofuatana  dhidi ya Biashara United na Dodoma jiji kabla ya kurudiana na RS Barkane katika michunao ya kombe la Shirikisho Afrika hivyo tunapaswa kuhakikisha wanashinda.

Akizungumzia mchezo dhidi ya Biashara utakaopigwa ijumaa katika dimba la Benjamini Mkapa, Pablo amesema utakuwa mchezo mgumu kutokana na uimara wa wapinzani hasa wanapokutana na timu kubwa.

“Biashara ni timu nzuri inacheza kitimu pia ina wachezaji wazuri mmoja mmoja, inapocheza na timu kubwa inatoa upinzani mkubwa lakini tutahakiksha tunapambana kupata ushindi uzuri ni kuwa tupo nyumbani na tutakuwa mbele ya mashabiki wetu”amesema.

Pia kwa upande wa Nahodha wa kikosi hicho John Bocco amesema akili za wachezaji wamezihamisha katika mechi hizo mbili za ligi kwanza kabla ya kukutana na Berkane.

“Tumerudi nyumbani tumeona tofauti ya alama dhidi ya Yanga tunahitaji kushinda ili kuendelea kuzipunguza na kuwapa presha vinara na kutimiza lengo la kutetea ubingwa wetu”amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here