Home SPORTS MSEMAJI WA SIMBA SC AMTEMBELEA SHEIK MKUU MUFTI ABUBAKAR BIN ZUBERY BIN...

MSEMAJI WA SIMBA SC AMTEMBELEA SHEIK MKUU MUFTI ABUBAKAR BIN ZUBERY BIN ALLY


 

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally hii leo amemtembelea nyumbani kwake Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Bin Zubeiry bin Ally

Katika ziara hiyo Ahmed amemkabidhi Mufti zawadi ya jezi na kumpa mwaliko wa kuhudhuria mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gendemarie utakaopigwa April 3 mwaka huu katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Akipokea zawadi hiyo Mufti ameeleza kufurahishwa ziara ya Meneja wa Simba na kueleza kuwa ameonesha heshima ya kuwathamini wakubwa

Kuhusu mwaliko wa kwenda uwanjani Mufti amesema amefurahi sana kwani ana muda mrefu hajaenda uwanjani na kama haitoshi mpira wa miguu unaondoa msongo wa mawazo

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here