Home BUSINESS MKUU WA WILAYA YA GEITA AWATAKA WAFANYA BIASHARA KUZALISHA BIDHAA ZENYE...

MKUU WA WILAYA YA GEITA AWATAKA WAFANYA BIASHARA KUZALISHA BIDHAA ZENYE UBORA.


Na: Costantine James, Geita.

Mkuu wa wilaya ya Geita mhe. Wilson Shimo amewataka wafanya biashara ndani ya wilaya ya Geita hasa wale wanaozalisha bidhaa zao wenyewe kuzalisha bidhaa zenye ubora zaidi kwa lengo la kuuza bidha zao kwenye masoko ya kitaifa/kimataifa pamoja na wadhabuni mbali mbali waliopo mkoa wa geita kwa lengo la kujiongezea kipato hali itakayochochea kukua kwa uchumi ndani ya wilaya ya Geita.

Kasema hayo katika kikao cha baraza la wafanyabiashara wilaya ya Geita kilichofanyika katika ukumbi wa GEDECO amewataka wafanya biashara ndani ya wilaya ya Geita kujikita katika uzalishaji wa bidhaa zenye ubora na zinazokubalika katika masoko mbalimbali hasa kitaifa na kimataifa kwa lengo la kuuza bidhaa zao hasa kwa wadhabuni mbalimbali waliopo mkoa wa Geoita.

Alisema wafanya baishara wilaya ya Geita wanayofursa kubwa katika kufanya biashara zao ndani ya wilaya ya Geita kwani wilaya hiyo pamoja na mkoa kwa ujmla unawadhabuni mbalimbali kama mgodi wa GGM, Bucreef hivyo wafanyabiashara wanatakiwa kutumia fursa kwa wadhabuni hao.

Mhe, Shimo amesema kuna changamoto kubwa kwa wafanyabiashara mbalimbali ndani ya wilaya ya Geita kupandisha bei za bidhaa zao  hali ambayo inapelekea wadhabuni na wateja mbalimbali  kwenda kutafuta bidha katika mikoa mingine hali inayopelekea serikali kukosa mapato.

“Sisi kama wana Geita tuendelee kuzalisha bidhaa ambazo soko lake linakwenda kupatikana kwenye kwenye fursa ambapo migodi yetu hii mikubwa inafanyakazi na inamahitaji ya bidhaa mbalimbali kama chakula rai yangu kwa wanaozalisha waendelee kuzalisha bidhaa ambazo nzuri na zakiwango  lakini tunayochangamoto ambayo inaendelea kujitokeza kwamba baadhi ya bidhaa ambazo zinapatikana hapa Geita zinakuwa zina bei ya juu na bei kubwa kulikohata ambavyo ungeweza kuagiza nje ya mkoa rai yangu kwa wafanya baishara bidhaa ambazo zipo Geita ziendele kuwa na bei ambayo inavutia wateja na si kuwakimbiza wateja wanakimbilia mikoa mingine” Amesema Wilson Shimo mkuu wa wilaya ya Geita.

Kwa upande wao wafanyabiashara mbali mbali walioshiriki katika kikao hicho wameiomba serikali kuwapunguzia mashariti katiaka upande wa urasimishaji biashara zao ili waweze kurasimisha biashara zao huku wakiomba mamlaka ya mapato nchini Tanzani TRA mkoa wa Geita kuwapatia elimu zaidi juu ya ulipaji kodi iliwaweze kulipakodi kwa lengo la kuchangia mapato kwa serikali.

“Nilikua nashauri kwa upande wa wafanyabiashara wadogo serikali iwezekutuangalia mashariti ya wafanyabiashara yapunguzwe  vigezo na mashari ya kuweza kurasimisha biashara zao yapunguzwe pia wafanya biashara wengi sio tu Geita wamekuwa hawajaelimishwa zaidi juu ya kodi kwahiyo serikali inatakiwa kuzingatia kwamba kila mfanyabiashara anakuwa na elimu ya kutosha juu ya ulipaji kodi” Alisema Bertha Joseph Makamu mwenyekiti biashara TCCIA mkoa wa Geita

Previous articleMAGAZETI YA LEO J.NNE MACHI 1-2022
Next articleMAFUNZO YA UVIKO 19 KWA WADAU WA SEKTA YA UTALII YAZINDULIWA JIJINI MBEYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here