Home LOCAL MIRADI YA IMF IKAMILIKE KABLA YA 30 JUNI, 2022; PROF...

MIRADI YA IMF IKAMILIKE KABLA YA 30 JUNI, 2022; PROF MAKUBI



Na: WAF-Songea 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ameagiza miradi yote ya Wizara  ya Afya chini ya Mfuko wa fedha wa kimataifa (IMF) iwe imekamilika kabla ya 30 Juni, 2022. 

Prof. Makubi ameyasema  hayo mkoani hapa alipotembelea mradi wa ujenzi wa  Hospitali mpya ya Rufaa ya mkoa huo,  

“Naagiza nchi nzima miradi yote ya IMF kwenye sekta ya afya inayosimamiwa na wizara ya afya iwe imekamilika tarehe 30 juni, 2022 , nje ya hapo ni kukaidi maagizo ya Viongozi na masharti ya matumizi ya Fedha hizi na tutakuondoa”

Aidha, Prof. Makubi amewataka uongozi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma kukaa na mkandarasi , ofisi ya Katibu Tawala Mkoa, Mshauri elekezi na Watalaamu wa Majengo toka wizara ya Afya kuhakikisha mradi wa ujenzi wa hospitali hiyo unakamilika kabla ya mwezi wa sita kuisha,

“Kakaeni pamoja, ule mradi watu wafanye kazi saa ishirini na nne , mkandarasi  aongeze wafanyakazi , waweke taa za usiku wafanye kazi usiku na mchana ili wakabidhi kabla ya mwezi wa sita haujaisha” alisisitiza Prof. Makubi

Kwa upande mwingine Prof. Makubi amewapongeza uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma kwa kufanya vizuri kitaifa katika eneo la chanjo dhidi ya UVIKO -19
Previous articleKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YAKAGUA MRADI WA UJENZI WA LANGO LA NAABI NA SERENGETI MEDIA CENTRE
Next articleSTAMICO YAELEZEA MAFANIKIO WALIYOYAPATA SIKU 365 ZA RAIS SAMIA MADARAKANI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here