Homeafya habari MGODI WA NORTH MARA WACHANGIA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50
MGODI WA NORTH MARA WACHANGIA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50
Daktari Mkuu wa Barrick North Mara, Dkt. Nicholaus Mboya akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya masuala ya UKIMWI.
Meneja wa Mahusiano ya Kijamii wa Barrick North Mara,Gilbert Mworia akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya masuala ya UKIMWI.
Mkuu wa wilaya ya Tarime,Kanali Michael Mntenjele akiongea wakati wa kikao hicho
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya bunge ya masuala ya UKIMWI wakifuatilia maelezo ya watendaji wa Barrick wakati wa ziara hiyo.
Tangu ianze kumiliki na kudhibiti uendeshaji wa mgodi wa dhahabu wa North Mara mnamo mwaka 2019, kampuni ya Barrick Gold Corporation (NYSE: GOLD) (TSX: ABX), imefanikiwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa zaidi ya nusu miongoni mwa wafanyakazi wa mgodi na jamii zinazozunguka mgodi huo kutoka kiwango cha juu cha 3.3% mwaka 2018 hadi 1.5% mwaka jana.
Wakati huo, maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) yamepungua kutoka kiwango cha juu cha 16% mwaka 2018 hadi 10% mwaka 2021, wakati kiwango cha magonjwa yote ya zinaa yamepungua kutoka asilimia 4.78% mwaka 2017 hadi 2.95% mwaka 2021.