Home ENTERTAINMENTS MAMBO NI MOTO SHEREHE ZA MIAKA 10 YA KATTY COLLECTON

MAMBO NI MOTO SHEREHE ZA MIAKA 10 YA KATTY COLLECTON


NA:MWANDISHI WETU

MIONGONI mwa sherehe ambazo watu wengi wamekuwa wakipenda kusherekea ni kumbukizi ya kuzaliwa ama kuanzishwa kwa taasisi, kikundi na kampuni inapotimiza kipindi fulani haswa iikiwa na mafanikio.

Katty Collection ni kampuni ambayo imejikita katika tasnia ya mitindo ya mavazi hususa ya kiafrika ilianzishwa na mbunifu wa mavazi Titty Morris, mwishoni mwa wiki hii watasherekea miaka10 ya kampuni hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Anasema jina la Katty Collection ni muunganiko wa herufi za majina ya watoto wake wa wili wa kike pamoja na jina lake.

“Wakati natafuta jina nilichukua herufi zinazopatikana katika majina ya mabinti zangu wa wili kwa sababu nilipokuwa na anzisha hii biashara nilikuwa nashauriana nao kila hatu mpaka leo wanafaham kila kitu kinacho husu ofisi hii hata nisipo kuwepo wanaweza kuendesha ikasimama imara,” anasema Titty Morris.

Katika sherehe hiyo mgeni rasm atakuwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, pia kutakuwa na onyesho la mavazi kutoka kwa wabunifu wa tatu chipukizi na Katty Collection yaliyo tamba tokea kuanziashwa.

Faida na changamoto ndani ya miaka kumi.

Anasema ndani ya miaka 10 amepata tuzo mbili mbunifu bora wa mwaka 2021 katika tamasha la Swahili Fashion Week na Pawes Awards Women in Fashion and Beauty 2022 alitunukiwa South Africa.

Ame bahatika kufanya kazi na watu mbali mbali wakiwemo wasanii wa kubwa miongoni  mwao ni Nassebu Abduli ‘Daimond’ na Reyvan katika ngoma ya Salome, pia lavalava na Hamonise nao amesha wavalisha.

Anasema ugonjwa wa Korona umekuwa changamoto kwa sababu wateja wake wengi wanatoka nchi za nje pia wengine ni watanzania ambao wapo mahofisini walianza kufanya kazi nyumbani.

“Nina wateja kutoka nchi za nje kipindi cha korona niliwakosa wengine watanzania walikuwa wanafanya kazi nyumbani harusi nazo zilisitishwa ilikuwa ni kipindi kigumu kwangu.”

Kurudisha kwa jamii.

Anasema katika sherehe za miaka kumi ya mafanikio ya Ketty Collection, atazindua mpango wa kusaidia mabinti na vijana wanaotaka kuanza kujikita katika tasnia ya mitindo.

“Nitatoa cherehani 100 kwa wanawake na vijana ambao wanachipukia katika tasia hii ila hawana mtaji mpango huu nitaufanya ndani ya miaka mitano nitauzindua rasm katika sherehe hii,” anasema Titty Morris.

Ateta na wabunifu wa Bongo

Anasema wabunifu wengi hawapendi kujitangaza katika kazi zao wamekua waoga kutumia kazi zao wakati wana vipaji vikubwa.

Ameeleza kwa upande wake amefanikiwa kwa sababu asilimia 80 ya nguo anazo vaa ameshona mwenyewe hii ni njia kubwa ya kujitangaza bila hata ya kutumia gharama kubwa.

Pia amesisitiza wabunifu kutobadili majina yao wanayo anzia kazi kubaki katika jina moja ili kutoyumbisha wateja, Pia kuweka nembo kwenye vitendea kazi vyao ikiwemo vifungashio vya nguo kwa wateja na kutumia vizuri mitandao ya kijamii.

Anasema hapa nchini anawakubali wabunifu Ally Rehmtula na Binjuu kwa sababu wanajituma katika kazi japo wapo wengi ambao nao anawapenda.

Aidha amesema nguo za wabunifu zinakuwa bei ya juu kutokana na mazingira ya kazi kwa mfano: wanalipa kodi laki mbili, kulipia leseni ya biashara, kujisajili Basata, ila mafundi wa kawaida unakuta ameweka cherehani kibarazani halipi kodi hata kama ubora wa nguo utakuwa sawa bei haziwezi kufanana.

Akoshwa na Mtasubiri ya Daimond na Zuchu.

Titty Morris ni mama wa watoto wa wili wa kike mmoja yupo chuo na mwengine shule ya sekondari.

Mbali na mambo ya mitindo taaluma yake ni uhasibu amefanya kazi katika kampuni na taasisi mbalimbli alipo acha kazi akaamua kujikita katika ujasiria mali.

Muda mwingi anapenda kusikiliza muziki na kwa kipindi hichi anapenda ngoma ya Daimond na Zuchu Mtasubiri ambayo ipo katika Ep ya Foa.

Mbali na muziki anapenda kuogelea pia ni shabiki wa mpira wa miguu kwa hapa nchin ana shabikia timu ya Simba.

Hapendi kuangalia filamu kwa sababu ana hisia za karibu mara nyingi akiangali kama ni ya kuudhunisha huwa ana lia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here