Home LOCAL MAFUNZO YA UVIKO 19 KWA WADAU WA SEKTA YA UTALII YAZINDULIWA JIJINI...

MAFUNZO YA UVIKO 19 KWA WADAU WA SEKTA YA UTALII YAZINDULIWA JIJINI MWANZA


Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Dkt. Shogo Mlozi Sedoyeka Akizungumza kwenye ufunguzi rasmi wa mafunzo ya siku tano ya UVIKO 19 kwa wadau wa Sekta ya Utalii katika Mkoa wa Mwanza yaliyozinduliwa Machi 7,2022 Katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jijini Mwanza.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mkuu wa Wilaya ya Magu Salum Kalli. akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel.
 

Dkt. Naiman Mbise Mratibu wa Mafunzo kwa watoa huduma katika mnyororo wa Sekta ya Utalii akizungumza alipokuwa akitoa hotuba ya utangulizi juu ya Mafunzo hayo.


Muongozaji wa hafla hiyo Elina Makanja akizungumza wakati alipokua akitagaza ratiba ya shughuli hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Dkt. Shogo Mlozi Akizugumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalum mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya ufuguzi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Dkt. Shogo Mlozia Sedoyeka (kulia) akijadiliana jambo na Mratibu wa Mafuzo hayo Mkoa wa Mwanza Dkt. Cuthbert Mero (kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mafunzo hayo katika Mkoa wa Mwanza. (PICHA NA: HUGHES DUGILO).

Na: Hughes Dugilo, MWANZA.

Katika kuhakikisha shughuli za Sekta ya Utalii nchini zinarejea na kuendelea baada ya kuathiriwa na janga la UVIKO-19, Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kutoa mafunzo kwa watoa huduma za utalii nchini Serikali kupitia Chuo cha Taifa cha Utalii chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kutoa mafunzo kwa watoa huduma katika Sekta ya Utalii nchini, ambapo jumla ya watoa huduma  150  katika Mkoa wa Mwanza  wanatarajia  kupatiwa mafunzo ya siku tano yanayohusu mwongozo wa kukabiliana na Uviko-19 katika sekta hiyo kuanzia Machi 7 hadi 11 mwaka huu JiJini Mwanza.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Dkt Shogo Mlozi Sedoyeka, amesema kuwa Chuo hicho  kinaendelea kutoa mafunzo hayo ambayo yamefadhiliwa na MPANGO WA MAENDELEO KWA USTAWI WA TAIFA NA MAPAMBANO DHIDI YA UVIKO-19,  kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii na kwamba mafunzo hayo yanatolewa katika mikoa nane ya  Tanzania Bara ikiwemo Lindi, Mtwara, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Njombe, Mwanza, na Mara, ambapo Mpaka Sasa tayari yameshatolewa katika mikoa sita na kwamba mikoa ya Mwanza na Mara ndio yamezinduliwa rasmi na  kukamilisha idadi ya mikoa yote nane ifikapo Machi 11, 2022.

Dkt.Sedoyeka amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wanarudisha shughuli za utalii katika hali yake ya awali na kufikia malengo ya taifa ya kufikia watalii milioni  5 ifikapo mwaka 2025, kwa sababu ya janga la UVIKO-19  liliathiri sana sekta ya utalii.

Amesema UVIKO-19 iliathiri kwa kiwango kikubwa Sekta hiyo na watalii kupungua kutoka  milioni 1.5 mwaka 2019 hadi  620,000 ambapo serikali kupitia chuo hicho imefanya jitihada mbalimbali ikiwemo ya kutoa mafunzo hayo.

Aidha amefafanua kuwa serikali ilitoa fedha hizo kwa ajili ya mafunzo hayo ambayo yamelenga kuwajengea uwezo watoa huduma wa Sekta hiyo  na kupata uelewa wa namna ya kufanya shughuli zao kwa kufuata miongizo na kuchukua tahadhari katika kukabiliana na janga la UVIKO-19.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Wilaya ya Magu Salum Kalli, amesema Sekta ya Utalii imechangia kuongeza fedha za kigeni kwa  taifa kwa  asilimia 25 na zaidi ya asilimia 17 katika Pato la taifa pia kuchangia ajira milioni 1.6.

Kalli amesema,janga la UVIKO-19 limeathiri sekta ya utalii duniani ambapo kwa hapa nchini imeshuka pia, kuyumba kwa biashara za utalii kwa sasa katika sekta ya utalii nchini imeanza kukamilika.

Amesema serikali katika kutambua umuhimu wa sekta hiyo imeamua kutafuta suluhu za changamoto ambapo kupitia chuo cha Taifa cha Utalii kimeanza mafunzo kwa wadau wa utalii.

“Sekta ya utalii ni muhimu katika kukuza pato la taifa,fursa kwenu kualika wawekezaji waweze kuwekeza mkoani Mwanza katika sekta ya utalii kwani tunajukumu la kukuza mji wa Mwanza  kwa kutengeneza  fukwe ndani ya ziwa Victoria,” amesema Kalli.

Mwisho

PICHA MBALIMBALI ZA MATUKIO KATIKA UFUNGUZI WA MAFUNZO HAYO


 
 



LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here