Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Puma Energy Tanzania Dkt. seleman Majige (wa sita kulia) akiwa na uongozi wa Kampuni hiyo pamoja na baadhi ya wadau waliopata tuzo katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa hafla ya utoaji wa Tuzo hizo zilizofanyika Machi 24,2022 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washindi wa Tuzo hizo wakipokea Tuzo zao kutoka kwa mgeni rasmi.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Puma Energy Tanzania Dkt. seleman Majige akitoa tuzo kwa moja wa wauzaji wa mafuta kwenye vituo vya puma kwenye sherehe za utoaji tuzo zilizofanyika Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Puma Energy Limited Tanzania Dominic Dhanah akizungumza mbele ya watoa huduma na wasambazaji mafuta hawapo pichani. Katika sherehe za utoaji Tuzo zilizofanyika Machi 24,2022 Jijini Dar es Salaam.
Meneja Mauzo ya Rejareja wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania Limited Venessy Chilambo akizungumzia mchakato waliopia kuwapata washindi mbalimbali wa Tuzo hizo.
DAR ES SALAAM
Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Limited Tanzania imesema kuwa itaendelea kuthamini mchango wa watoa huduma wao ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika biashara na kwamba jamii imeendelea kunufaika na huduma bora kutoka kwa watoa huduma hao.
MWENYEKITI wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Limited nchini Tanzania Dkt. Seleman Majige ameyasema hayo kwenye hafla ya utoaji Tuzo kwa wasambazaji na watoa huduma ya mafuta huku akitangaza rasmi mkakati wa Kampuni hiyo kuanza kuuza Nishati ya Gesi ya Majumbani kupitia vituo vyao vyote vya Mafuta hivi karibuni.
Dkt..Majige Amesema kuwa kwakuwa kampuni ya Mafuta ya Puma Energy ndio namba moja na yenye huduma bora hapa nchini hivyo hata kwenye uuzaji na usambazaji wa Nishati hiyo ya Gesi watakuwa namba moja Kama ilivyo kawaida yao.
Mwenyekiti huyo wa Bodi ameyasema hayo wakati sherehe wa kutoa tuzo hizo ambao umefanyika katika ukumbi wa Golden Jubilee Mkoani Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mwakilishi kutoka Hazina, wafanyabiashara pamoja na wasambaji na watoa huduma kote nchini.
“Nawapongeza wote mliopata tuzo hizi na kwakweli tunajivunia kwa huduma bora ambazo unazifanya na niwaombe mkaendelee kuitangaza, na kuilinda Puma Energy limited ili iendelee kuwa kampuni namba moja kwa ubora. “Amesema Dkt Majige
Nakuongeza kuwa hivi karibuni tunakwenda Kuaza kufanya huduma ya Biashara ya usambazaji Gesi ya majumbani kwani tayari Bodi imeshakaa na kupitisha hilo hivyo matarajio yangu nikuona tunaendelea kuwa namba moja kwa ubora wa huduma zetu hivyo nawapongeza nyote kwa kazi nzuri mnayofanya. “amesisitiza Mwenyekiti Majige
Pia akizungumzia Kampuni hiyo amesema kuwa wameendelea kuwa namba moja kwani kila kituo ambacho utakwenda utakuta huduma hiyo ya mafuta na hivi sasa wameongeza vituo kutoka 52 vya awali nakufikia vituo 80 lakini lengo nikuona hadi kufikia mwaka 2025 wanakuwa na vituo 150 na sio 100.
“Niombe Menejimenti ya Kampuni hii ya Puma kwamba hadi kufikia mwaka 2025 muwe mmeongeza vituo hadi kufikia 150 na sio 100 kama mlivyokuwa mmepanga mimi naamini tunaouwezo wa kufikia vituo 150 hivyo tujielekeze huko kwani uwezo upo na muhakikishe vituo hivyo vinafikia. “Amesema Dkt. Majige
Dkt Majige amewaeleza wadau hao na kuwakumbusha Kuwa Puma ni kampuni kubwa hivyo waendelee kuilinda na kuhakikisha mafuta yanakuwa salama lakini pia ameitaka menejimenti kuweka mkakati wa kuaziasha vituo vijijini ili kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wananchi wengi zaidi.
Amemaliza kwa kuendelea kuwakumbusha watoa huduma kutumia maneno mazuri kwa wateja kwani hiyo ndio silaha ya Puma energy kuendelea kuwa namba Moja na kwakufanya hivyo kutawafanya wateja kufurahia huduma zao Kama ilivyokawaida.
Awali wakati akimkaribisha mgeni rasmi Miurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Limited Tanzania Dominic Dhanah Amesema Kampuni hiyo ndio inayoongoza nchini na inashika namba moja kwa ubora.
Amesema kuwa namba moja ni kazi kubwa sana lakini wataendelea kuwekeza nakwamba hadi kufikia sasa Puma inavituo 80 kutoka vituo 52 vilivyokuwepo hapo mwanzo na lengo nikufikisha vituo 100 kufikia mwaka 2025.
“Ndugu Mgeni rasmi kampuni imeendelea kuwa wabunifu na tumeongeza huduma nyingine ya vilainishi vya kwenye magari na mapema mwaka huu tunatarajia kuzindua nishati ya gesi ya majumbani ambayo itakuwa inapatikana kwenye vituo vyetu vyote na hakuna shaka kwamba itapokelewa vizuri. “Amesema Dhanah
Pia amewapongeza watoa huduma wote wa Puma energy nakusema kwamba wao ndio chachu ya mafanikio ya kampuni hiyo huku akiwataka kuendelea kuendelea kufanya vizuri zaidi na katika tuzo hizo kituo cha mafuta kutoka Arusha cetral station kimefanikiwa kuwa mshindi wa jumla wa uuzaji wa mafuta na hiyo ni mwaka wa pili mfululizo.
Katika tuzo hizo washiriki walifanikiwa kupata tuzo ya vikombe na pesa taslimu sh.laki 2.5 kama motisha na kuwapa hamasa ya kuendelea kufanya vizuri zaidi.
Mwisho.