Home LOCAL KAMATI YA SIASA MKOA WAPONGEZA MIRADI INAYOTEKELEZWA WILAYANI SIKONGE.

KAMATI YA SIASA MKOA WAPONGEZA MIRADI INAYOTEKELEZWA WILAYANI SIKONGE.

Na: Lucas Raphael,Tabora

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi amewataka watendaji wa serikali wilayani kuhakikisha miradi ya Maendeleo inakamilika kwa wakati na Viwango ili kuleta  tija kwa wananchi.

Kauli hiyo ilitolewa wakati  wa kamati ya siasa ya mkoa wa Tabora ilipofanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya Sikonge mkoani hapa.

Alisema kwamba Kamati ya Siasa Mkoa wa Tabora inawajibika kuangalia na kukangua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika wilaya zote ilikuona thamani ya fedha ilivyotumika kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Hassan Wakasuvi aliipongeza Wilaya ya Sikonge kwa ujenzi wa Viwango vinavyotakiwa pamoja na usimamizi mzuri ya miradi hiyo na thamani halisi ya fedha zilizotolewa na serikali zimetumika vizuri na kuonesha tija kwa wananchi.

Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Tabora Wakasuvi imekagua ujenzi wa Vyumba 3 vya madarasa ya UVIKO-19  uliogharimu shilingi Milioni 60 katika Shule ya Sekondari Kamagi na kuwapongeza  kuwa fedha hizo zimetumika vyema.

Aidha Kamati ilikagua mradi wa ujenzi wa wodi ya wazazi ,Kituo cha Afya Tutuo uliogharimu shilingi Milioni 250, ikiwa ni fedha za tozo za miamala ya Simu mradi ambao unatarajiwa  kukamilika ifikapo  Machi 25,2022.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Sikonge John Palingo aliipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi za miradi ya Maendeleo kwa kipindi cha Mwaka mmoja  wa Uongozi wake katika Sekta mbalimbali ikiwemo Afya,Elimu,Maji na Miundombinu ya Barabara .

Previous articleRAIS SAMIA SULUHU HASSAN APOKEA TAARIFA YA KIKOSI KAZI CHA KURATIBU MAONI YA WADAU WA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI VYA SIASA,IKULU DAR ES SALAAM
Next articleZUTH ZAIPUNA:TUNAADHIMISHA MWAKA MMOJA WA MAFANIKIO MAKUBWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here