Home BUSINESS KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAIPONGEZA STAMICO KWA...

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAIPONGEZA STAMICO KWA MRADI WA MKAA MBADALA

Na: Bibiana Ndumbaro, DAR ES SALAAM.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wametembelea  na kukagua kiwanda cha kuzalisha mkaa mbadala wa makaa ya mawe  (Rafiki Briquettes)  kilichopo Msasani, jijini Dar es salaam.

Kamati hiyo ilitembelea kiwanda hicho siku tarehe 14 Machi 2022 na kupokelewa na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Madini  na Shirika la Madini la Taifa wakiongozwa na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa,  Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo.

Akiongea mara baada ya kutembelea kiwanda na kujionea jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi Mwenyekiti  wa Kamati  hiyo Mhe. Dustan Kitandula ameipongeza STAMICO kwa kuwa na ubunifu ambao unalenga kuchangia katika jitihada za kutunza mazingira, kuongeza ajira na kuongeza nishati ya kupikia.

Amesema ubunifu  wa STAMICO ni mkubwa na unahitaji pongezi kwa kuwa unakuja kuchangia  katika ongezeko la nishati  kidigitali nchini.

Amesema STAMICO  inatakiwa kuongeza  kasi na kukamilisha taratibu za uzalishaji ili iweze kuipeleka bidhaa hii sokoni kwa kuwa ina uhutaji mkubwa sana sokoni

Aidha ameitaka STAMICO kutanua wigo wa soko kwa kufanya  kampeni ya kutosha ili watumiaji waweze  kupata taarifa  zaidi kuhusu  mkaa huu, sambamba  na kuainisha changamoto  zinazorudisha nyuma kasi ya uzalishaji  ili kuweza kutatua changamoto  hizo kwa pamoja .

Naye Naibu Waziri wa Madini Dkt.Kiruswa ameishukuru Kamati kwa kutembelea mradi huo muhimu na kushukuru kwa ushauri na maelekezo yaliyotolewa yakilenga kuujenga mradi huo ili uwe imara zaidi.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse alipata fursa ya kutoa taarifa ya mradi pamoja na faida zake zikiwemo kuongeza mapato  ya Shirika, kuokoa misitu, kuchangia kodi,  kutoa ajira na kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Aidha, amekiri kuyatekeleza maoni na maelekezo yote yaliyotolewa na Waheshiwa Wabunge.

Viongozi wengine walioshiriki kwenye ziara hii ni pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Madini na STAMICO, Mameneja na wataalamu kutoka STAMICO ambao ndio wasimamizi mradi huo.

Previous articleLETSHEGO AFRICA PRESS RELEASE
Next articleAbsa Group 2021 Earnings Increase on Lower Impairments, Higher Pre-prevision Profit
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here