Timu ya Geita Gold FC yenye masikani yake mkoani Geita imetamba kuimaliza timu ya wananchi Yanga Sc katika mchezo wao wa ligi kuu Tanzania bara unaotarajiwa kupigwa March 6. 2022.
Mchezo huo utapigwa katika Dimba la Ccm kirumba mkoani siku ya jumapili March 6 katibu mkuu wa Timu hiyo Simon Shija amesema kikosi kipo kinaendelea vizuri kujiandaa na mchezo huo ili kuhakikisha wanavuna alama zote tatu.
Akizingumza katika mkutano na waandishi wa Habari Mjini Geita Katibu wa Geita Gold Fc Simon Shija amekanusha pia taarifa za madai ya kuuza mechi yao dhidi ya timu ya Yanga Sc, Amesema habari hizo ni za mtaani ambazo hazina nia njema na timu hiyo.
Ameeleza kuwa Geita Gold imejipanga vizuri kwa ajili ya mechi hiyo na maandalizi yote yamekamilika huku akiwataka mashabiki watimu hiyo kujitokeza kwa wingi kununua tiketi kwa lengo la kujitokeza kwa wingi kuja kuishangilia timu yako ili ipate ushindi.
Shija amesema sababu za kupeleka mchezo huo katika dimba la Ccm kirumba ni usalama wa mashabiki wa timu zote mbili kwani wamehofia mashabiki kujaa katika uwanja wao wa Nyankumbu stadium hali ambayo ingepelekea msongamano mkubwa katika uwanja huo.
Katika mchezo wa awali Geita Gold Fc ailipoteza kwa kipigo cha bao moja kwa sifuri dhidi ya yanga mchezo uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam hivyo katika dimba la Ccm kirumba watahakikisha wanavuna pointi zote ili kuzidi kijiweka sehemu mzuri katika msimamo wa Ligi kuu ya NBC.