Home LOCAL DG LUDIGIJA ATAKA WAZABUNI WASIO NA VIWANGO KUNYIMWA TENDA

DG LUDIGIJA ATAKA WAZABUNI WASIO NA VIWANGO KUNYIMWA TENDA

 

Na: Heri Shaaban Ilalah ,erishaban@gmail.com

MKUU wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija ameagiza  Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam  kuwanyima tenda wazabuni wasio na viwango katika miradi ya maendeleo Ilala.

Mkuu wa Wilaya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija ametoa agizo hilo katika ziara yake ya kukagua Miradi ya Maendeleo akiwa na kamati ya ya Ulinzi na Usalama Wilaya llala.

“Naagiza Halmashauri  msiwape tenda wazabuni wasio na viwango watakwamisha kazi ya ujenzi wa miradi yetu ambayo inatekelezwa na fedha za Serikali muwape tenda wazabuni wenye sifa

Ludigija alisema wazabuni wenye sifa wakipewa tenda  katika miradi mikubwa ya Serikali ujenzi wake unakwenda kwa haraka  kazi zinahisha kwa wakati.

Katika ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo Leo Jimbo la SEGEREA LUDIGIJA alikagua ujenzi wa kituo cha afya , Kiwalani, Kinyerezi na Segerea ambapo aliwataka  wajenzi wa miradi  hiyo kujenga kwa kufuata taratibu za ujenzi na ubora unaotakiwa .

Ludigija aliagiza Kamati za ujenzi zote kusimamia Miradi hiyo na kutoa ushirikiano.

Ludigija alipongeza mradi wa kituo cha afya Kinyerezi ambapo ujenzi wake umejengwa kwa mapato ya ndani  umefika hatua nzuri.

Msaidizi wa Mbunge wa Jimbo la Segerea Rutha Lucharaba alipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanikisha ujenzi wa miradi mikubwa Jimbo la Segerea, Kiwalani, Kinyerezi na Segerea vituo hivyo vya Afya vitatu vikikamilika vitakua mkombozi Katika kuwasaidia Wananchi wa eneo hilo.

Rutha Lucharaba alisema mradi wa kituo cha afya Kiwalani ukikamilika kitatumiwa na Wakazi wa Kata ya Minazi Mirefu ambayo aina kituo afya,Aidha kituo Cha Afya Cha kisasa kinachojengwa Kata ya  Segerea kikikamilika kitatumiwa na Kata ya Kimanga ,Liwiti na meneo ya jirani .

Mhandisi wa Halmashauri ya Jiji John Magori alisema Kila mradi wa afya wa Serikali fundi mmoja , Mafundi wote wanawasimamia wanaojenga kwa kiwango na kufuata Taratibu

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here