Home LOCAL DC KILOSA AWASIMAMISHA KAZI WENYEVITI 3 WA VITONGOJI KWA MATUMIZI MABAYA MADARAKA

DC KILOSA AWASIMAMISHA KAZI WENYEVITI 3 WA VITONGOJI KWA MATUMIZI MABAYA MADARAKA

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alahj Majid Mwanga amewasimamisha kazi wenyeviti wa vitongoji vitatu kwa makosa mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya madarakani.

DC Mwanga amewataja wenyeviti hao waliowaondoa madarakani ni Kondo Pilipili Kitongoji Cha Masugu Kati,John Kalonga Kitongoji Cha Masugu,Ally Liguta Kitongoji Cha Mitalulani.

Wenyeviti hao wamesimamishwa kwa makosa ya mbalimbali ikiwemo Kuuza maeneo ya hifadhi ya misitu zaidi ya hekari 70 pamoja na mashamba ya wananchi kwa wafugaji kinyume na Sheria ya ardhi

Adha katika hatua nyingine amemtaka mtendaji wa kijiji Cha Dodoma Isanga Andrew Kazimbaya kuripoti ktk ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilosa ili akapangiwe majukumu mengine kwa kushindwa kisimamia majukumu na sheria katika kijiiji hicho.

Pia amewaagiza wataalamu wa Kata ya Magomeni wakiongozwa na Mtendaji wa kata, Afisa Maendeleo ya Jamii, Afisa Mifugo na Afisa Kilimo waandae taarifa ya kina juu ya migogoro iliyosababishwa na wenyeviti na kuiwasilisha ofisi ya mkuu wa wilaya ndani ya siku Saba.

Aidha amesisitiza umujimu wa ujezi wa shule ya msingi ktk vitongoji hivyo kwani watoto wanatembea umbali mrefu kufuata shule umbali mrefu.

Previous articleRAIS SAMIA SULUHU HASAN AFUNGUA RASMI DARAJA LA TANZANITE PAMOJA NA BARABARA UNGANISHI JIJINI DAR ES SALAAM
Next articleOFISI YA RAIS-UTUMISHI YDHAMIRIA KUWA YA KWANZA KUKAMILISHA UJENZI WA OFISI ZA KUDUMU KATIKA MJI WA SERIKALI ILI KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here