Home ENTERTAINMENTS DAR ES SALAAM FASHION WEEK YAJA NA ‘EVENING CONNECTION PARTY’ KWA WADAU...

DAR ES SALAAM FASHION WEEK YAJA NA ‘EVENING CONNECTION PARTY’ KWA WADAU WA MITINDO


NA: MWANDISHI WETU

MUANDAAJI wa onyesho la mavazi la Dar Es Salaam Fashion Week Clement Mdindilwa ‘Clemoo Desgner’, amesema kuwa jukwaa hilo lina tofauti kubwa na majukwaaa ambayo yamewahi kufanyika hapa nchini.

Onyesho hilo ambalo linatarajiwa kufanyika Septemba 23 hadi 25 jijini Dar Es Salaaam, ambapo wabunifu zaidi ya 30 ndani na nje ya nchi wataonyesha kazi zao.

Akizungumza na ukurasa huu amesema tamasha hilo ni la tofauti kwa sababu wabunifu watapata elimu kutoka kwa wabunifu wa kubwa kutoka nje ya Tanzania.

“Tamasha hili limejikita katika kukutanisha wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi kujifunza soko la kimataifa siku ya kwanza tutafungua tamasha kwa mazungumzo na semina siku hiyo tumeipa jila la ‘Evening Connection Party’ hii itaendeshwa na wabobezi wa tasnia wenye mafanikio makubwa ndani na nje ya bara la Afrika,” anasema Clemoo.

Aliongeza pia kutakuwa na mnada wa kuuza bidhaa ambazo zimetengenezwa na wabunifu ambao watakuwa wamejisajili kuonyesha kazi zao katika tamasha hilo.

Aidha alitoa wito kwa wabunifu wa ndani ambao bado hawajafanya usahili wa kushiriki katika onyesho hilo kukamilisha usajili wao kwa kutembelea mitandao ya kijamii ya au kufika katika ofisi za Clemoo Desgner zilizopo Ilala Sharifu Shamba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here