Home LOCAL BALOZI WA UFARANSA NABIL HAJALOUI NA MABALOZI WENGINE WA EU WATOA MSIMAMO...

BALOZI WA UFARANSA NABIL HAJALOUI NA MABALOZI WENGINE WA EU WATOA MSIMAMO WAO JUU YA VITA YA UKRAINE NA URUSI

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam (hawamo pichani) wakati wa mkutano na waandishi hao uliowahusisha mabalozi wengine wa Umoja wa Ulaya  (EU) (hawamo pichani) kuhusu msimamo wao juu ya vita kati ya Ukraine na Urusi.


Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui (katikati) akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawamo pichani) kuhusu mapigano yanayoendelea baina ya Ukraine na Urusi . (kushoto), ni Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Manifredo Fanti, na (kulia), ni Balozi wa Poland nchini Tanzania Krzysztof BUZALISKI. Mkutano huo umefanyika Machi 22,2022 katika Makazi ya Balozi wa Ufaransa Jijini Dar es Salaam na kuudhuriwa na Mabalozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania.

 

Balozi wa Umoja wa Ulaya Manifredo Fanti (katikati) akizungumza wakati wa Mkutano huo akieleza jitihada zinazofanywa na Umoja huo kuhakikisha vita ya Ukraine na Urusi inamalizika.

Balozi wa Poland nchini Tanzania Krzysztof BUZALISKI, (katikati) akizungumza katika mkutano huo kuelezea namna ambavyo nchi yake ilivyojitolea kuhakikisha wakimbizi wanaokimbia vita na kuingia poland wanapokelewa na kupewa hifadhi.

Baadhi ya Mabalozi kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania wakisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa mkutano huo uliofanyika katika makazi ya Balozi wa Ufaransa Machi 22,2022 Jijini Dar es Salaam.

Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria katika mkutano huo wakifuatilia taarifa inayotolewa na Mabalozi wa Umoja wa Ulaya juu ya Msimamo wa nchi zao kuhusu mapigano yanayoeendelea kati ya Ukraine na Urusi. Mkutano huo umefanyika katika makazi ya Balozi wa Ufaransa Machi 22,2022 Jijini Dar es salaam. PICHA NA: HUGHES DUGILO.

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.
BALOZI wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui pamoja na Babalozi wengine wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) amezungumzia mapigano yanayoendelea kati ya Ukraine na Urusi katika kuhakikisha amani inarejea katika nchi hizo kwa njia ya mazungumzo ili kuepuasha madhara zaidi yasiendelee kutokea.

Balozi Hajlaoui ameyasema hayo Machi 22,2022 alipokutana na waandishi wa habari akiwa pamoja na Mabalozi wa nchi wanachama wa Umoja huo katika makazi yake yaliyopo katika Ubalozi wa Ufaransa JIjini Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa Ufaransa na nchi zilizopo katika Umoja huo wanasimama na Ukraine kuhakikisha vita hiyo inamalizika na nchi hizo mbili kukaa pamoja kufanya mazungumzo ya amani na kwamba jitihada ni katika kuhakikisha hakuna madhara zaidi yatakayoweza kutokea.
 
Aidha Balozi Hajlaoui amesema kuwa mnamo Machi 2,2022 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio linaloitaka Urusi kusitisha mara moja matumizi ya nguvu dhidi ya Ukraine katika kura iliyoidhinishwa kwa wingi na nchi 141 ikiwa ni pamoja na nchi zote wanachama wa Umoja wa Ulaya huku nchi tano zikipinga na nchi 35 kuacha kupiga kura Kati ya wanachama 193 wa Jumuiya.

“Urusi imeanzisha vita bila uchokozi wowote na ukiukwaji mkubwa wa sheria za Kimataifa na ahadi zake zote,nchi 27 wanachama wa EU zimepitisha vikwazo vikubwa dhidi ya Urusi . Jumuiya inasikitishwa na matumizi makubwa ya nguvu yanayotumika kuishambulia Ukraine,”amesema Balozi Hajlaoui.

Ameongeza kuwa EU imeamua kuweka vikwazo vya moja kwa moja kwa watu wanaohusika na maamuzi yanayohusiana na vita lakini pia mfumo wa kiuchumi wa umma na wa kibinafsi wa Urusi ambao unaunga mkono juhudi hizo za vita na kwamba katika upande wa kifedha Urusi iko karibu kuondolewa kwenye masoko ya kifedha.

“Vikwazo hivyo pia vitakuwepo katika kuzuia Uwekezaji wote katika sekta ya nishati ya Urusi na utangazaji wa vyombo vya habari ambavyo vinarudisha propaganda za vita vya Urusi katika EU. Tayari vikwazo hivyo vimeanza kufanya kazi,”ameongeza Balozi Hajlaoui.

Aidha amesema kuwa EU iko tayari kuongeza shinikizo zaidi ili kuongeza ukali wa vita kwa Urusi na kuifanya nchi hiyo kuamua kusitisha mapigano  na kufikia mazungumzo kama Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alivyotangaza katika mkutano wa wakuu wa nchi za Ulaya wa Versailles Machi 10-11 mwaka huu.

Katika taarifa ya pamoja ya Ufaransa na EU inaeleza kuwa wanachama wa Umoja huo wanaunga mkono kufunguliwa kwa uchunguzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai katika mashambulizi ya Urusi na kusababisha madhahara makubwa kwa Raia wakiwemo majeruhi.
 
“Hata hivyo Rais Emmanuel Macron anaendelea na mazungumzo na Vladimir Putin ili kupata suluhisho la amani katika mgogoro huo” inaeleza taarifa hiyo.

katika hatua nyingine Balozi Nabil pamoja na Umoja wa Ulaya wametoa ombi kwa nchi za Afrika ikiwemo Tanzania kutoa kauli kwa Urusi ili iwezeshe kusitisha vita dhidi ya Ukraine na kwamba nchi za Afrika zinatambua madhara yanayopatikana kutokana na vita hiyo.

Previous articleDC MKUDE AKAGUA UJENZI WA MIRADI YA MAJI KISHAPU KILELE WIKI YA MAJI…ATAKA RUWASA IONGEZE KASI, WANANCHI WATUMIE MAJI SAFI NA SALAMA
Next articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHIYA LEO J.TANO MACHI 23-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here