Home LOCAL ARUSHA: WAZIRI UMMY AKIPONGEZA KITUO CHA SANAA TANZANIA KWA KUWAPA WALEMAVU AJIRA.

ARUSHA: WAZIRI UMMY AKIPONGEZA KITUO CHA SANAA TANZANIA KWA KUWAPA WALEMAVU AJIRA.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiongea baada ya kutembelea kituo cha Sanaa Tanzania kinachofanya kazi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali Kwa kutumia watu wenye ulemavu.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiangalia moja ya bidhaa inayotengenezwa na watu wenye ulemavu alipotembelea SanaaTanzania wingine ni mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo.

Meneja wa Sanaa Tanzania Sasuia Bruins akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na kazi wanazofanya walemavu katika kampuni hiyo.

Picha ya pamoja kati ya waziri wa Afya Ummy Mwalimu na viongozi mbalimbali pamoja na watu wenye ulemavu wanaofanya kazi Sanaa Tanzania

NA: NAMNYAK KIVUYO,ARUSHA.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amekipongeza kituo cha Sanaa Tanzania  kwa kuwapa walemavu   ajira ya kutengeneza thamani za ndani na vitu mbalimbali ikiwemo urembo ambapo ajira hiyo inayowasaidia kupata kipato na kuweza  kujikimu kimaisha  

Waziri Ummy alitoa pongezi hizo wakati alipotembelea kituo hicho ambapo alisema kuwa kinachofanyika ni jambo kubwa na zuri kwani angalau walemavu hawa wakiondoka hapo mwisho wa mwezi wana uhakika wa kupata mshahara unaoenda kuwasaidia angalau kupata mahitaji yao ya nyumbani.

“Mimi niwaombe mfanye kazi kwa bidii kwa bidii na kwa kujituma lakini pia msije mkasema kwamba ndio mmefika mwisho bali muwe na ndoto kubwa wengine mnaweza mkaja kumiliki maduka makubwa ya kutengeneza vifaa mbalimbali vya nyumbani,”alisema Ummy Mwalimu.

Alifafanua kuwa Rais Samia Suluhu Hassan kupitia mfuko wa watu wenye ulemavu ameshawaelekeza kila halmashauri kutenga asilimia mbili kupelekwa kwa watu wenye ulemavu hivyo viongozi mbalimbali wafanye wajibu wao kutekeleza agizo hilo lakini pia kufanya vizuri kama Sanaa Tanzania.

Kwa upande wake Meneja wa Sanaa Tanzania Sasuia Bruins alisema kuwa wanachukua watu ambao hakuna mtu anawataka na vitu ambavyo hakuna watu wanaovitaka na kutengeneza vitu ambavyo watu wanavinunua Duniani kote hivyo wanaoenda kufanya kazi na watu wenye ulemavu kwani wanauwezo mkubwa wakati mwingi kuliko watu wasio na ulemavu wa aina wowote.

“Wanaowezo mkubwa  hata zaidi ya watu wasio na ulemavu wowote labda ni kwasababu wana kiu ya kufanya kazi na kuwa huru bila kisaidiwa na mtu mwingine, mimi kwakweli toka nianze kufanya kazi na walemavu hawa nimeona wana uwezo mkubwa,”alisema Meneja huyo.

Aidha aliwasihi watanzania na jamii kwa ujumla kujaribu kuwakaribisha watu wenye ulemavu katika  makampuni yao kwani wataona na kufurahia wanachokifanya kwani wana akili na uwezo mkubwa wa kufanya kazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here