Home BUSINESS WAFANYABIASHARA ZA MTANDAO WAJITOKEZA USAJILI WA BRELA JIJINI DAR

WAFANYABIASHARA ZA MTANDAO WAJITOKEZA USAJILI WA BRELA JIJINI DAR




Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

WAKALA wa Usajili wa Biahara na Leseni (BRELA) umesema kuwa moja ya mikakati yake katika mwaka huu 2022 ni kuhakikisha wanakwenda katika mikoa na wilaya zote hapa nchini ili kuwafikia wananchi katika maeneo yao kwa lengo la kuwapa Elimu na Huduma kwa lengo la kutatua changamoto zinazoikabili.

Akizungumza kwenye mahojiano na Waandishi wa habari katika viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam, Afisa Leseni wa BRERA Robert Mashika amesema kuwa katika siku tano za awali walizoweka Kambi ya utoaji Elimu na Huduma viwanjani hapo wamebaini changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ambapo wengi wao wamekuwa wakisumbuliwa na mifumo ya kimtandao.

Adha amesema katika kipindi cha siku tano za zoezi hilo wamewahudumia wananchi zaidi ya 1000 waliojitokeza kupata Elimu na Huduma za Usajili wa Biashara zao na kwamba kutokana na uhitaji wa wananchi wa huduma zao BRELA ikachukua hatua ya kuongeza muda wa siku tatu hadi Februari 2, mwaka huu.

“Moja ya mikakati ya BRELA kwa mwaka huu ni kuwafuata wananchi katika maeneo yao, tutakwenda kila Mkoa, kila Wilaya ilimradi kila mtu awe na elimu ya usajili” amesema Mashika. Na kuongeza kuwa

“Tunataka tunavyoenda huko mbele biashara zote ziwe zimesajiliwa, watu wasije kusema wamekosa usajili ,kila aina ya biashara inatakiwa kusajiliwe. ameoneza

Amebainisha kuwa katika zoezi linaloendelea viwanjani hapo wamebaini Biashara nyingi zinazofanywa kwa njia ya mtandao na kwamba kuna wananchi wengi waliojitokeza kufanya usajili wa Biashara hizo.

“Ziko Biashara nyingi zinazofanyika Online ambazo zinatakiwa kusajiliwa ,na wengi ambao wamefika kuhudumiwa hapa ni wale wanaofanya biashara kwa njia ya online” amebainisha.

Ametoa rai kwa wananchi kujitahidi kufahamu namna ya kutumia mifumo yao ya kimtandao kutokana na shughuli nyingi za BRELA ziko kwenye mifumo hiyo na kwamba ni ngumu kukwepa mifumo hiyo isipokuwa kwa kupitia elimu wanayotoa kwa wananchi katika maeneo mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here