Home BUSINESS WADAU WANAOSHIRIKI MAFUNZO YA UVIKO – 19 KATIKA SEKTA YA UTALII WAOMBA...

WADAU WANAOSHIRIKI MAFUNZO YA UVIKO – 19 KATIKA SEKTA YA UTALII WAOMBA MAFUNZO HAYO YAWE ENDELEVU

Mkuu wa Idara ya Ukarimu na Mkufunzi Mwandamizi katika Sekta ya huduma kwa wateja na Mapokezi Jesca Willium akiendelea na mafunzo kwa wadau wa mnyororo katika sekta ya Utalii Wilayani Ruangwa.
Mkuu wa Idara ya Uratibu na Matukio na mkufunzi mwandamizi katika Sekta ya upishi Chuo cha Taifa cha Utalii Mary Maduhu akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.
 
Mkufunzi kutoka Chuo cha Taifa cha Utalii Naomi Kyando akitoa mada jinsi watoa huduma wanavyoweza kutatua na kushughulikia malalamiko ya wateja na pia wanavyoweza kutunza na kusimamia muda wao vizuri ili kuhakikisha wanatoa huduma bora katika kipindi hiki cha UVIKO -19.

Mkufunzi kutoka Chuo cha Taifa cha Utalii Caeserena Rusanyu akifundisha somo la usalama wa chakua na usafi katika eneo la kazi na mazingira kwa ujumla katika mafunzo ya siku tano yanayoendelea Wilayani Ruangwa, Mkoani LIndi. (PICHA NA: HUGHES DUGILO).

Na: Hughes Dugilo, RUANGWA.

Wadau wanaoshiriki Mafunzo ya watoa huduma katika Mnyororo wa Utalii kupitia Mradi wa UVIKO 19 awamu ya kwanza yanayoendelea Wilayani Rangwa Mkoani Lindi wameiomba Serikali kupitia Chuo cha Taifa cha Utalii kuweka utaratibu wa kuwapelekea mafunzo hayo mara kwa mara ili kuendelea kuwajengea uwezo katika maeneo mbali mbali katika Sekta hiyo.

wakiongea kwa nyakati tofauti walipofanyiwa mahojiano baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru Serikali kwa kuendelea kuchukua hatua katika kukabiliana na janga UVIKO 19 na kwamba uwepo wa mafunzo hayo kutawajengea uwezo wa kufahamu namna ya kukabiliana na janga hilo.

Hamisi Slim Othman ni mshiriki wa mafunzo hayo, ameeleza kuwa janga la UVIKO 19 limekuwa tishio hasa katika sekta ya Utalii na kwamba ujio wa mafunzo hayo yamekuwa na tija kubwa kutokana na uwepo wa wageni wanaoingia nchini na kupata huduma katika maeneo mbalimbali ya nchi.

“Sisi kwa niaba ya Serikali ya Wilaya ya Ruangwa tumefarijika sana kiasi ambacho hatuna cha kuilipa Serikali tumeweza kuona kumbe kuna muingiliano baina ya kuona huduma zetu na hili wimbi la UVIKO – 19 tunakishukuru sana Chuo cha Taifa cha Utalii kutuletea Mafunzo haya tumenufaika sana kwa kufahamu namna gani ya kuwahudumia wageni wanaofika katika maeneo yetu ya kazi” amesema Othman.

Nae mshiriki mwingine wa mafunzo hayo mjasiriamali Lesa Rogers, amesema kuwa amenufaika sana na mafunzo hayo na kwamba elimu hiyo ataitumia kwa kuwaelimisha watu wengine waliokosa fursa hiyo na kwamba amefarijika sana kupata chanjo ambayo inatolewa kwa hiyari katika mafunzo hayo.  

“Chuo cha Taifa Cha utalii tunakishukuru kutuletea mafunzo haya mimi kama Mjasiriamali nimenufaika sana kwa kufahamu vitu vingi kuhusu UVIKO 19 hata sasa naweza kuwafundisha na wenzangu namna ya kujikinga na Ugonjwa huu” amesema Lesa Rogers.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Ukarimu na Mkufunzi Mwandamizi katika Sekta ya huduma kwa wateja na Mapokezi Jesca Willium amesema kuwa mafunzo hayo yanayoendelea Wilayani Ruangwa yamelenga katika kuwajengea uwezo washiri hao kufahamu mbinu mbalimbali wanazoweza kuzitumia katika kipindi hiki cha UVIKO -19 na kutambua namna ya kutoa huduma zao na kushughulikia changamoto za wateja kwa ujumla.

“Leo tumeendelea na Mafunzo ambapo washiriki wameweza kujengewa uwezo wa mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya usafi sehemu zao za kazi na wao wenyewe kama watoa huduma kwa kutambua kuwa ni jinsi gani usafi unavyoweza kuwa suluhisho katika kipindi hiki cha UVIKO 19 na usalama wa chakula kwa ujumla” amesema Jesca.

Mafunzo hayo ya siku tano yanayoratibiwa na Chuo cha Taifa cha Utalii yanawakutanisha wadau mbalimbali wa sekta hiyo kutoka katika wilaya zote za Mkoa wa lindi na kuendelea katika mikoa nane ya Tanzania Bara.

PICHA MBALIMBALI ZA WASHIRIKI WA MAFUNZO.


Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI ASUBUHI YA LEO J.TANO FEBRUARI 9-2022
Next articleWAJUMBE 308 BODI ZA VYUO VYA UALIMU 35 NCHINI WAPIGWA MSASA ADEM BAGAMOYO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here