Home SPORTS SIMBA YATAKATA KWA MKAPA, YAICHAPA ASEC MIMOSAS 3 -1

SIMBA YATAKATA KWA MKAPA, YAICHAPA ASEC MIMOSAS 3 -1

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

MABINGWA wa ligi Kuu Simba leo wameibuka na ushindi wa bao 3-0 dhdi ya ASEC Mimosas katika Michuano ya  Kombe la Shirikisho, uliopigwa dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam

Katika dakika 12   Pape Sakho aliipatia timu yake bao baada ya kupokea  pasi ya Shomari Kapombe lililodumu mpaka muda wa mapumziko.

Katika kipindi cha pili ASEC Mimosas walifanya kweli na kupata bao la kusawazisha dakika ya 60 kupitia kwa Aziz Stephan ambaye alitumia vema makosa ya safu ya ulinzi wa Simba chini ya Joash Onyango na Enock inonga. 

Bao la pili kwa Simba lilipachikwa na Kapombe ambaye alifunga kwa mkwaju wa penalti matata katika dakika ya 78.

Iliwachukua dakika tatu mbele Simba kupachika bao la tatu kupitia kwa Peter Banda ambaye alionyeshwa kadi ya njano kutokana na kuvua jezi wakati anashangilia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here