Home SPORTS SIMBA YAICHAPA RUVU SHOOTING 7-0

SIMBA YAICHAPA RUVU SHOOTING 7-0

Mwandishi wetu

MABINGWA watetezi, Simba SC leo wametinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa ushindi wa 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba SC yamefungwa na Nahodha, John Bocco mawili dakika ya pili n 40, Clatous Chama matatu dakika ya 23, 25 na 73, Masinda aliyejifunga dakika ya 44 na Jimson Mwanuke dakika ya 70.

Simba imeungana na timubnyingine zilizofuzu Robo Fainali ni Azam FC Geita Gold , Coastal Union, Kagera Sugar,  Polisi Tanzania,  Yanga SC na timu pekee isiyo ya Ligi Kuu, Pamba.

Droo ya Robo Fainali itafuatia wiki ijayo na mechi za hatua hiyo ya Nane Bora zitachezwa mwezi ujao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here