Home SPORTS SIMBA QUEENS KUSHUKA DIMBANI KUIKABILI FOUNTAIN GATE LEO

SIMBA QUEENS KUSHUKA DIMBANI KUIKABILI FOUNTAIN GATE LEO

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Na: Stella Kessy.

MABINGWA watetezi Simba Queens leo wanashuka dimbani kuchuana na  Fountain Gate Princess kwenye uwanja wa Mo Simba Arena.

Mchezo huo ni   kiporo ambapo Fountain wachezeji wao wengi walikuwa katika timu ya taifa kushiriki katika michuano ya kukata tiketi ya kombe la Dunia.

Hata hivyo kikosi cha Simba Queens ndio vinara wa ligi kuu ya wanawake  pia endapo watashinda mchezo huo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza  watamaliza bila ya kufungwa, ( yaani watakuwa wameshinda mechi zote 11).

Hata hivyo  Fountain Gate Princess wakishinda watakuwa ndio timu pekee ambayo imevunja rekodi ya kutofungwa katika mzunguko wa kwanza.