Home BUSINESS SERIKALI YAWAJENGEA UWEZO WADAU JUU YA MKATABA WA AFCFTA JIJINI DAR

SERIKALI YAWAJENGEA UWEZO WADAU JUU YA MKATABA WA AFCFTA JIJINI DAR


Naibu Waziri wa Uwekezaji , Viwanda na Biashara Exaud Kigahe akizungumza katika ufunguzi wa akifungua warsha ya siku tatu ya kuwajengea wezo wadau mbalimbali kutoka Serikalini na Sekta Binafsi kuhusu Mkataba wa Eneo huru la Biashara la Afrika (AfCFTA)

Mkurgenzi Mkaazi wa Taasisi ya TMEA iliyofadhili Warsha hiyo Monica Hangi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mahojiano maalum na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika ratiba za ufunguzi wa Warsha hiyo. 


Dkt. Halima Noor Mshauri Mwandamizi wa AfCFTA akizungumza kwenye Warsha hiyo

Mkurugenzi wa Utafiti na Sera Taasisi ya Sekata Binafsi Tanzania (TPSF) Andrew Mahiga akizungmizia umuhimu wa wafanyabiashara kujiandaa kikamilifu kwa kurasimisha biashara zao.


Naibu Waziri wa Uwekezaji , Viwanda na Biashara Exaud Kigahe (kulia) akiwa na Mkurgenzi Mkaazi wa Taasisi ya TMEA iliyofadhili Warsha hiyo Monica Hangi (kushoto) wakizungumza mara baada ya kumalizika kwa ratiba ya ufunguzi waWarsha hiyo Jijini Dar es Salaam. (PICHA: NA HUGHES DUGILO).
Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Naibu Waziri wa Uwekezaji , Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amesema kuwa Nchi za Bara la Afrika zinaweza kujiimarisha kibiashara kwa kushughulikia changamoto katika maeneo muhimu ikiwemo miundombinu.

Ameyasema hayo leo Februari 14,2022 Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akifungua warsha ya siku tatu ya kuwajengea wezo wadau mbalimbali kutoka Serikani na Sekta Binafsi juu ya Mkataba wa Eneo huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) ili waweze kuchangamkia ipasavyo fursa za Masoko na Biashara pindi biashara itakapoanza kufanyika chini ya Mkataba huo.

“Matarajio yetu ni kufanya Warsha hizi katika maeneo mbalimbali nchini ili elimu hii iweze kufika kwa wadau wengi kadri iwezekanavyo kwa kuhakikisha wanashiriki ipasavyo katika kufanya Biashara kati ya nchi na nchi za Bara la Afrika” amesema Kigahe.

Adha amebainisha kuwa mchakato unaoendelea kwa sasa ni hatua nyingine ambayo serikali imekua ikifanya uchambuzi wa kina kuhusu mkataba huo kwenye uchumi wa nchi, na kuandaa mkakati wa Kitaifa wa AfCFTA ujulikanao kama (Nationali AfCFTA Strategy) ambapo Wataalam wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Mtaalam Mwelekezi wamezunguka katika maeneo mbalimbali ya nchi kupata taarifa na maoni ya wadau kuhusu utekelezaji wa Mkataba huo.

Amewataka Watanzania na wazalishaji wa Bidhaa hapa nchini kujiandaa kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kupata soko la uwakika kutokana na upinzani mkubwa wa bidhaa nyingi zitakazokuwa zikizalishwa kwenye nchi nyingine za bara la Afrika.

“Ukweli ni kwamba soko la AfCFTA, pamoja na fursa zitakazojitokeza huenda zikaleta upinzani wa biashara, hivyo ninaomba nichukue fursa hii kuwahimiza kuhakikisha kuwa tunaendelea kuzalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu ambazo zitaweza kuingia katika nchi nyingine za Afrika” alisisitiza Mhe. Kigahe.

Kwa upande wake Mkurgenzi Mkaazi wa Taasisi ya TMEA iliyofadhili Warsha hiyo Monica Hangi, amesema kuwa katika warsha hiyo pamoja na lengo kuu la kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa serikali na Sekta Binafsi, lakini pia kuhakikisha kuona kama nchi inapata manufaa ya Mkataba huo kwa kuangalia fursa zilizopo katika Mkataba huo.

“Unajua kwa sasa hivi Tanzana tuna wafanyabiashara wengi wanaangalia soko dogo lililopo hapa Tanzania na tuliingia ndani ya Afrika Mashariki Tukapanua Soko ambapo kuna nchi 6 tu, lakini kwenye soko hili la AfCFTA kuna nchi 55 kuna watu zaidi ya Bilioni 1 ambapo sisi kama watanzania tunaweza kupeleka bidhaa zetu na kuweza kupata fedha nyingi” Amesema Hangi.

Na kuongeza kua, “Nafasi hii tulioanzia leo ni nzuri sana kwa sababu huu mkataba umerasimishwa hivi karibuni kwa hiyo sisi tunachofanaya sasa ni kutengeneza uelewa kwa adau ili wale wanaotumia huu Mkataba waweze kuufanyia kazi” Ameongeza Hangi

Nae Mkurugenzi wa Utafiti na Sera Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Andrew Mahiga amesema kua Mkataba huo unatoa fursa kwa Taasisi yao kujipanga na kujiandaa kikamilifu hasa katika kupata uelewa kwani sasa ushindani wa biashara unakwenda kuongezeka kutokana na kuwepo bidhaa kutoka katika nchi nyingine, na kuhakikisha ubora wa bidhaa zenyewe unazingatiwa.

Pia amewashauri wafanyabiashara kurasimisha biashara zao ili kuwepo kwa mazingira bora ya kufanyia bashara.

“Kama unavyofahamu Biashara nyingi za hapa Tanzania ni za chini na za kati hivyo kama biashara yako sio rasmi hata ile bidhaa yako huwezi kupata uthibitisho wa ubora na pia huwezi kwenda kuuza nje ya nchi, hivyo sisi kama TPSF kazi yetu pia ni kuwaelimisha watu kuhusu hili soko linamaanisha nini na linataka nini na kuwahamasisha kurasimisha biashara zao ili wapate kile kiwango cha kufanya biashara Afrika nzima” amesema Mahiga.

Warsha hiyo hiyo ya Siku tatu iliyoanza leo inatarajiwa kufungwa rasmi siku ya jumaa tano Februari 16,2022.

 PICHA  MBALIMBALI ZA WASHIRIKI WA WARSHA HIYO.





 

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here