Home LOCAL SERIKALI ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA BORA NA WEZESHI KWA KUZINGATIA VIVUTIO VYA KIKODI...

SERIKALI ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA BORA NA WEZESHI KWA KUZINGATIA VIVUTIO VYA KIKODI KWA MIRADI MIKUBWA NA YA KIMKAKATI.


DODOMA.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaudi Kigahe (Mb.) amesema Serikali itaendelea kuboresha na kuweka mazingira bora na wezeshi kwa kuzingatia vivutio vya kikodi  kwa lengo la kuchochea  uwekezaji katika sekta mbalimbali za uchumi, kuongeza ajira, kupata fedha za kigeni, biashara za kimataifa  na kukuza uchumi.

Mhe. Kigahe ameyasema hayo wakati wa utoaji wa Taarifa  kuhusu utaratibu wa utoaji wa vivutio vya kikodi kwa miradi mikubwa ya kimkakati, mafanikio, changamoto na hatua za kukabaliana nazo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Bajeti, Februari 15, 2022  katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma. 

Akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Chande, Naibu Katibu Mkuu Uwekezaji – Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara  Bw. Ally Gugu na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na  Mipango Bw. Lawrence Mafuru, aliwahakikishia wajumbe wa Kamati hiyo kuyafanyia kazi maoni yote waliyotoa katika kuhamasisha na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kujenga uchumi endelevu. 

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Daniel Sillo (Mb.) amesema Wizara inatakiwa kuendelea kuweka vivutio muhimu mbalimbali kwa wawekezaji na kuvifuatilia kama vinatumika ipasavyo na kuonyesha matokeo chanya kwa ukuaji wa uchumi wa nchi.   

Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo walitoa maoni na mapendekezo yanayolenga kuboresha uwekaji wa vivutio vya kikodi, uwekaji wa kodi zinazofaa, kuimarisha usimamizi  na ufanyaji tathmini kwa vivutio vya kikodi vinavyotolewa, kuangalia kwa makini miradi ya kimkakati inayohitaji kodi, kuongeza muda kwa miradi ya kimkakati iliyobainishwa na  kuimarisha ulinzi wa wawekezaji wa ndani. 

Akitoa taarifa hiyo ya utaratibu wa utoaji wa vivutio vya kikodi kwa wajumbe wa kamati hiyo,  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uwekezaji  wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Aristides Mbwasi alisema katika utaratibu huo, Serikali imefanikiwa  kusajiri miradi 42 ya wawekezaji mahiri yenye thamani ya Dola za marekani billion 12.3 na kufanikiwa kutoa vivutio vya kikodi kwa wawekezaji mahiri na wawekezaji mahiri maalum kwa mujibu wa sheria.   

Previous articleZOEZI LA UWEKAJI ANWANI ZA MAKAZI LAANZA RASMI JIJI LA ARUSHA ,DKT PIMA ASEMA HAWATA MVUMILIA YOYOTE ATAKAYENDA KUHUJUMU
Next articleRAIS SAMIA AZUNGUMZA NA MABALOZI WA OACPS BRUSSELS NCHINI UBELGIJI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here