Home SPORTS SENEGAL YANYAKUA UBINGWA WA AFCON 2022, YAICHAPA MISRI KWA PENALT 4-2

SENEGAL YANYAKUA UBINGWA WA AFCON 2022, YAICHAPA MISRI KWA PENALT 4-2Na: Hughes Dugilo.

Timu ya soka ya taifa ya Senegal imefanikiwa kunyakua ubingwa wa fainali za Mataifa ya Afrika 2022 (AFCON) kwa kuichapa timu ya taifa ya Misri kwa mikwaju ya Penati 4 – 2 mchezo uliopigwa katika Dimba la Olembe Jijini Yaunde Cameroon.

Kwa mujibu wa takwimu timu ya Taifa ya Senegal imefanikiwa kuchukua ubigwa huo kwa mara ya kwanza toka ashiriki mashindano hayo na kwamba timu hiyo imewahi kucheza katika hatua ya fainali mara tatu mwaka 2012, 2019 na mwaka huu ambapo imefanikiwa kunyakuwa ubigwa.

Aidha timu ya Taifa ya Misri imeshuka Dimbani ikiwa ni mara ya tisa kucheza katika hatua ya Fainali ya michuano hiyo na kufanikiwa kubeba ubingwa mara saba.

Katika mchezo huo uliokuwa mkali kwa timu zote mbili kucheza kwa kushambuliana ilishuhudiwa mshambuliaji nyota wa Senegal Sadio Mane akikosa penati katika dakika za mwanzoni mwa mchezo huo baada ya beki wa Misri kucheza  madhambi katika eneo la hatari.  Hata hivyo pamoja na kukosa penati hiyo bado waliendelea kucheza kwa nguvu na kasi kubwa.

Mpaka mwamuzi anapuliza kipyenga cha mwisho cha dakika 90 hakukuwa na timu iliyoona lango la mwenzake na hivyo kuongezwa dakika 30 zilizokamilisha dakika 120 za mchezo huo kwa sare ya 0-0.

Mashindano hayo ya AFCON 2022 yalishirikisha jumla ya mataifa 24 ambapo jumla ya michezo 52 ilichezwa.

 

Previous articleWATU 206 WATHIBITIKA KUWA NA VIRUSI VYA CORONA NDANI YA WIKI MOJA
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI ASUBUHI YA LEO J.TATU FEBRUARI 7-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here