Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima amekutana na kufanya mazungumzo na Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Afya (MAB) kwa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) na Menejimenti ya mamlaka hiyo, walipokwenda Ofisini kwake wakati wa ziara yao ya kutembelea maeneo ya mipakani kuangalia uingizwaji wa bidhaa bandia katika maeneo hayo ambapo kwa Mkoa wa Tanga watatembelea Mpaka wa Horohoro. Kushoto kwa RC Malima ni Mwenyekiti wa MAB, Eric Shitindi na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo.