Home LOCAL RC GEITA AAGIZA KUMALIZIKA OPERESHENI YA ANWANI YA MAKAZI IFIKAPO APRILI 15,...

RC GEITA AAGIZA KUMALIZIKA OPERESHENI YA ANWANI YA MAKAZI IFIKAPO APRILI 15, 2022

Na: Costantine James, Geita.

Mkuu wa mkoa wa Geita Rosemary Senyamule amewataka wakazi wa mkoa wa Geita Kushiriki kikamilifu katika zoezi la operasheni anwani ya makazi ndani ya mkoa wa Geita  kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuchochea kukamilika kwa  wakati zoezi hilo ifikapo tarehe 15 Aprili 2022.

Alisema hayo wakati akizungumza na wakazi wa Nyankumbu mkoani Geita katika zoezi la uzinduzi wa operasheni ya anwani ya makazi iliyo ambatana na kaulimbiu ya “Mfumo wa anwani za makazi kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi” amesema zoezi hilo ni mhumu kwa jami kwani litarahisisha zoezi la sense ya watu na makazi inayotarajiwa kuanza mwezi Agosti 2022 hali ambayao zoezi hilo likikamilika litawezesha wananchi kufikiwa kwa urahisi katika makazi yao.

“kwanza tumshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa uthubutu wa kuanza kutekeleza jambo hili kwani kwa miaka yote tumekuwa tukifanya sensa ya watu bila makazi lakini kwa hatua hii tutasonga mbele. Pia, niwaombe wananchi kuwa tayari kwani baada ya uzinduzi huu kutakuwa na wiki moja ya kutoa elimu kisha kuchagua majina na kuyabandika kwenye Mitaa. Muhimu ni kuhakikisha wakurugenzi mnatumia rasilimali zilizopo ili kufanikisha zoezi hili ndani ya miezi miwili kutoka tarehe ya leo” Alisema Mhe. Rosemary Senyamule  Mkuu wa mkoa waq Geita. 

Katibu Tawala Msaidizi Mipango na urwtibu mkoa wa Geita alisema kuwa mfumo wa anwani ya makazi uliopo Tanzania ni sanduku la posta lakini kutokana na maendeleo ya teknologia matuzi yake yameanza kupungua huku akisema zoezi hili la anwani ya makazi linamanufaa makubwa kwa wananchi ikiwemo kurahisha huduma za ulinzi na usalama kwa wananchi.

“Katika swala huli la anwani ya makazi kuna manufaa ambayo yanapatikana manufaa hayo ni kurahisisha huduma za ulinzi na usalama, nikuongeza ufanisi katika usimamizi wa makazi na watu, nikuwezesha mkutambua mali na kaya kaitka eneo furani furani, ni kurahisisha upatikanaji wa takwimu mbali mbali kuongeza tija na ufanisi katika huduma za uokoaji na maafa kuwezesha ukusanyaji wa kodi mbali mbali kwa urahisi kwa wakati kuongeza kasi ya kupambana na uhalifu, ufanisi katika kupata taarifa za uhamiaji na kuongeza ufanisi katika shughuli za utalii pamoja na kurahisha mawasiliano kati ya serikali na wananchi kwa makusudi mbali mbali”. Alisema Deodatus Kayango katibu Tawala msaidizi mipango na uratibu mkoa wa Geita.

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa katika kurahisisha zoezi hili viongozi mbali mbali mbali wa serikali katika mkoa wa geita  wanatakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kujenga uelewa na uwezo kuhusu anwani za makazi kwa wananchi.

“Katika operesheni hii ya uandaji wa anwaniza makazi kuna hatua mbali mbali ambazo zinztakiwa zifanyike, kujenga uelewa na uwezo kuhusu mfumo wa anwani za makazi kwa makundi tofauti ikiwemo waheshimiwa madiwani, watendaji wa kata na mitaa wenyeviti wa mitaa na vijiji kuhusu uelewa wa mfumo anwani za makazi kwa upande wa kundi hilo vile vile kunakutambua majina ya barabara, mitaa na kuhakikisha mitaa yote na barabara inakuwa na majina kazi hii itafanywa na watendaji wa kata na wenyeviti wa mitaa” Alisema Deodatus Kayango katibu tawala Msaidizi mipango na uratibu mkoa wa Geita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here